News China: Marufuku kutembea na mbwa hadharani

China: Marufuku kutembea na mbwa hadharani

-

Kaunti moja nchini China huko Yunnan imelazimika kufikiria tena sera ya kupiga marufuku wakazi wa eneo hilo kutembea na mbwa katika maeneo ya umma kuanzia Novemba 20.

Taarifa hiyo imesema, yeyote atakayekutwa anatembea na mbwa hadharani mara tatu, mbwa wake atachukuliwa na mamlaka na kuuawa.

Maafisa wamesema hiyo ni hatua ya kulinda wakazi kwasababu kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mbwa kuuma watu.

Hata hivyo, sera hiyo imekasirisha watu katika mitandao ya kijamii huku maafisa wakisema huenda “wakafikiria tena” hatua hiyo.

Taarifa hiyo inasema kuanzia Novemba 13, itakuwa ni lazima kwa wamiliki wote kusalia na mbwa wao nyumbani muda wote.

Pia imeongeza kwamba sera hiyo inatoa muongozo mzuri wa kuishi na mbwa.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Georgia elections official urges Trump to rein in supporters

A senior Georgia elections official on Tuesday called on President Donald Trump to rein in his supporters, lashing out...

US investigates potential bribery and lobbying schemes for pardons

The US Justice Department is investigating whether there was a secret scheme to lobby White House officials for a...

Barr appoints special counsel in Russia probe investigation

Attorney General William Barr has given extra protection to the prosecutor he appointed to investigate the origins of the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you