News Dk. Mwinyi atoa miezi mitatu kwa uongozi wa hospital...

Dk. Mwinyi atoa miezi mitatu kwa uongozi wa hospital ya Mnazi mmoja

-

RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa Wizara ya Afya kurekebisha kasoro za kiutendaji zinazosababisha kutokuwepo  ufanisi katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo  wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja, alipofika kuangalia utoaji wa huduma kwa wagonjwa katika maeneo na vitengo  tofauti  vya Hospitali hiyo.

Alisema kwa kiwango kikubwa mambo mengi yanahitaji kufanyiwa marekebisho, akibainisha kuwepo changamoto mbali mbali za kiutendaji na hivyo kuzorotesha uapatikanaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Alisema analenga kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watendaji wasiowajibika kazini na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ukosefu wa huduma, pamoja na kupewa lugha zisizordhisha kutoka kwa wauguzi na watendaji wengine  wa Hospitali hiyo.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema pamoja na Serikali kuipatia fedha za kutosha Hospitali hiyo kila mwezi, kumekuwepo changamoto za ukosefu wa vifaa muhimu kwa wagonjwa ikiwemo magodoro, dawa na vifaa vya maabara, hivyo akautaka Uongozi wa Hospitali hiyo kubadilika na kuondokana na utendaji wa mazowea.

Alisema pale Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na hatimae wagonjwa wakakosa dawa hizo, ni dhahiri kuwa kuna tatizo mahala hapo.

Alieleza kuwa kumekuwepo matatizo madogo madogo katika uendeshaji wa Hospitali hiyo na kubainisha  kuwa; kama yangelishuhulikiwa ipasavyo , ni wazi kuwa huduma bora zingepatikana.

Aidha Rais Dk. Mwinyi , aliahidi kufanya ziara nyingine katika siku zijazo na kuzungumza na wafanyakazi kwa lengo la kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Alisema wafanyakazi wana wajibu wa kuwatumikia wagonjwa kikamilifu sambamba na kupata haki wanazostahili.RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa Wizara ya Afya kurekebisha kasoro za kiutendaji zinazosababisha kutokuwepo  ufanisi katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo  wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja, alipofika kuangalia utoaji wa huduma kwa wagonjwa katika maeneo na vitengo  tofauti  vya Hospitali hiyo.

Alisema kwa kiwango kikubwa mambo mengi yanahitaji kufanyiwa marekebisho, akibainisha kuwepo changamoto mbali mbali za kiutendaji na hivyo kuzorotesha uapatikanaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Alisema analenga kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watendaji wasiowajibika kazini na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ukosefu wa huduma, pamoja na kupewa lugha zisizordhisha kutoka kwa wauguzi na watendaji wengine  wa Hospitali hiyo.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema pamoja na Serikali kuipatia fedha za kutosha Hospitali hiyo kila mwezi, kumekuwepo changamoto za ukosefu wa vifaa muhimu kwa wagonjwa ikiwemo magodoro, dawa na vifaa vya maabara, hivyo akautaka Uongozi wa Hospitali hiyo kubadilika na kuondokana na utendaji wa mazowea.

Alisema pale Serikali inapotoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na hatimae wagonjwa wakakosa dawa hizo, ni dhahiri kuwa kuna tatizo mahala hapo.

Alieleza kuwa kumekuwepo matatizo madogo madogo katika uendeshaji wa Hospitali hiyo na kubainisha  kuwa; kama yangelishuhulikiwa ipasavyo , ni wazi kuwa huduma bora zingepatikana.

Aidha Rais Dk. Mwinyi , aliahidi kufanya ziara nyingine katika siku zijazo na kuzungumza na wafanyakazi kwa lengo la kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Alisema wafanyakazi wana wajibu wa kuwatumikia wagonjwa kikamilifu sambamba na kupata haki wanazostahili.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Exports from Fars province up 30% in eight months amid virus

The Director-General of Fars Customs  Office announced, "Since the beginning of the current Iranian calendar year on March 20...

Hezbollah files lawsuits against accusations on Beirut blast

The Arabic-language NNA network cited Lebanese lawmaker Ibrahim al-Mousawi as saying that Hezbollah has filed two lawsuits against a former...

People going out over weekend urged to remain cautious

People have been urged to remain cautious and stick to Covid guidelines as restaurants and gastro pubs across the...

‘The 11th Step’ wins at Polish film festival

The film, won the best prize at the Children section of the event, which was held online on November, 23-28....

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you