News Halmashauri ya vijiji Tarime kujenga vyoo kila soko kunusuru...

Halmashauri ya vijiji Tarime kujenga vyoo kila soko kunusuru jamii na magonjwa ya mlipuko

-

Na Timothy Itembe Mara.

Halmashauri ya Tarime vijijini imejipanga kujenga vyoo kila soko na minada ili kuwanusuru wananchi wake na magonjwa ya mlipuko.

Akiongea na waandishi wa habari,Afisa Afya wa halmashauri hiyo,Mjaya Bwire Ofisini kwa mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri,  alisema mradi huo utatekelezwa kupitia  mapato ya ndani.

Bwire alisema kuwa ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko yanayosababisha rasilimali nyingi kupotea halmashauri yake imejipanga kujenga vyoo kila soko na minada kupitia mapato ya makusanyo ya ndani.

“Mradi huo wa ujenzi wa vyoo umeanza ndani ya vituo vyetu vya Afya na tutaenda mbali zaidi ambapo tumepanga kujenga vyoo katika masoko na minada ili kujenga jamii yenye Afya Bora na maendeleo endelevu”alisema Bwire.

Kwa upande wake Kaimu usafi wa mazingira wa halmashauri hiyo,Martha Mahule alisema kuwa halmashauri yake imejenga vyoo ndani ya vituo vya Afya zaidi ya 4 na ndani ya masoko na minada taklibani 6.

Mahule aliongeza kusema kuwa anatarajia kuona wananchi wanamwitikio wa kutoa ushirikiano na kupiga vita maradhi huku wa kizingatia  sheria na taratibu za mazingira na za kiavya.

Naye mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri alisema usafi wa kitaifa wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi unaenda vizuri kwa wilaya Tarime na jamii inamwitikio mkubwa. 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

No doubt Zionist regime behind terror of Fakhrizadeh

TEHRAN, Nov. 29 (MNA) – Washington Post quoted a senior US official as saying that Zionist regime is definitely...

Health Minister says Covid vaccine could be rolled out by early 2021

Vaccines could be made available to Irish residents early in the New Year, the Minister for Health Stephen Donnelly...

Cuban FM slams terrorist assault against Iranian Scientist

Reacting to the assassination of Mohsen Fakhri Zadeh, the prominent Iranian nuclear scientist, Cuban Foreign Minister Bruno Rodriguez wrote...

Egypt: Countries must reach binding deal on Nile dam

Amid regional tension over the project, countries along the Nile must reach a legally binding agreement on the filling...

Karua, Itumbi Fault BBI Signature Collection Tactics 

Senior Counsel Martha Karua and Digital Strategist Dennis Itumbi have called out the national government for allegedly using taxpayers...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you