News Jurgen Klopp amuonya Salah kuhusu corona

Jurgen Klopp amuonya Salah kuhusu corona

-

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amezungumza na mshambuliaji wa klabu hiyo Mohamed Salah kuhusu miendendo yake baada ya kupatikana na virusi vya corona mara mbili aliporejea kutoka shughuli ya kimataifa nchini Misri.

Kiungo huyo mwenye miaka 28-aliripotiwa kuonekana akicheza densi katika harusi ya ndugu yake.

Salah, ambaye kwa sasa amejitenga, aytakosa meshi ya Jumapili dhidi ya viongozi wa Ligi Leicester na pia huenda akakosa mechi ya Champions League dhidi ya Atalanta.

Klopp amesema Salah alirejea siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa uhusiano wake na mchezaji huyo ni “mzuri”.

Mjerumani huyo ameongeza kuwa: “Yuko hali nzuri na anaendelea kupata nafuu.

“Hakuna la kusema hadharani kuhusu mambo ninayojadiliana na wachezaji wangu lakini naweza kuwafahamisha kwamba msimu wa joto nilikuwa Ujerumani na rafiki yangu aliahirisha hafla ya siku ya kuzaliwa kwa mwanawe kwasababu nilikuwa huko.

“Ilikuwa inahudhuriwa na watu 50. Ilikuwa inafanyika nje lakini niliamua kutohudhuria dakika za mwisho.

“Katika nchi zingine kuna shinikizo za kijamii,harusi ya ndugu yake ni siku muhimu sana. Kile ninachoweza kusema kwa ujumla ni kwamba wachezaji wangu ni wazuri na wana nidhamu. Kuna baadhi ya visa vinatokea lakini sote tunafahamu hali zingine haziepukiki.

Salah amefunga mabao 10 katika mechi 13 ya mashindano yote msimu huu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Nine freezer lorries arrive in Ireland to assist with Covid vaccine rollout

Nine Covid-19 ultra-low freezer lorries have arrived in the country to assist in the rollout of the Pfizer/BioNTech vaccine. The...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you