News Kaseja na wenzake warejea kikosini kuendelea na maandalizi ya...

Kaseja na wenzake warejea kikosini kuendelea na maandalizi ya mchezo wao na Azam

-

 

Nahodha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC ,Juma Kaseja pamoja na David Brayson wameungana  na wachezaji wenzao leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu Soka Tanzania bara ikiwa ni baada ya kutoka katika kikosi cha Timu ya Taifa Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu kombe la Afrika (AFCON 2021).

Mbalina Kaseja, Brayson ,wengine waliorejea kuungana na kikosi cha KMC FC ni Kocha wa Magolikipa wa timu hiyo, Fatuma Omary ambaye aliitwa kufundisha magolikipa wa Timu ya Taifa ya Wanawake U-17 katika michuano ya kuwania ubingwa wa kombe la COSAFA.

Aidha KMC FC hivi sasa inaendelea kufanya maandalizi katika kuelekea mchezo wa mzunguko wa 12 wa ligi kuu ambapo itakutana na Azam Jumamosi ya Novemba 21 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo.

Hata hivyo katika kikosi hicho, wachezaji wawili bado hawajarejea kambini ambao ni pic Ally ambaye alifiwa na Baba yake mzazi  pamoja na Rahim Sheihe ambaye bado yupo katika Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Aidha hadi sasa kikosi cha KMC FC hakina majeruhi na kwamba mchezaji ambaye alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Gwambina Misungwi Mkoani Mwanza , Emmanuel Mvuyekule amesharejea mazoezini na kwamba anaendelea vizuri hadi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Hugging friends and family over Christmas an ‘extreme risk’

The head of the HSE has warned that hugging friends and family over the Christmas period poses an “extreme...

Padri Atuhumiwa Kumpa Mimba Mwanafunzi

Erasmus Swai (44), ambaye ni Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Manushi, Jimbo la Moshi, anatuhumiwa kumbaka na kumpa...

Mr Price store in Carlow can sell groceries but not food, court rules

Dunnes Stores has secured a High Court injunction preventing a rival retailer from continuing to sell food products, but...

What Sonko’s Impeachment Means For Nairobi

The impeachment of Nairobi Governor Mike Sonko by the county assembly cast a shadow of uncertainty over the future...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you