News Kauli ya Guardiola juu ya Lionel Messi hii hapa

Kauli ya Guardiola juu ya Lionel Messi hii hapa

-

Kocha wa Manchester City, Pep Guadiola amesema angependa kuona Lionel Messi akimalizia maisha yake ya soka kwenye klabu yake ya Barcelona ya Hispania kwakuwa ana maelewano mazuri ya kihistoria na klabu hiyo.

“Ninachotaka ni Messi amalizie maisha yake ya soka Barcelona. Napenda iwe hivyo, Natamani itokee. Lakini msimu huu atamalizia mkataba wake na sijui nini kitatokea kwenye akili yake. Ila kwasasa ni mchezaji wa Barcelona siwezi sema zaidi”.

Suala la Guadiola kuhusiwa kumsajili Messi limeibuka upya ikiwa ni siku mbili tokea anasaini kandarasi ya miaka 2 kuendelea kuifundisha Man City hadi mwaka 2023 huku ikiripotiwa Messi hana furaha hivi sasa na miasha ndani ya klabu yake hivyo anaweza akatimka na kuungana na Guadiola.

Messi na Guadiola wamewahi kufanya kazi pamoja kwa miaka minne wakati Guardiola alipokuwa anakionoa kikosi hicho na kusaidia kwa kiasi kikubwa kukuza kiwango cha mchezaji huyo na kuifanya Barcelona kushinda mataji 14 ikiwemo mataji matatu makubwa kwa msimu ‘Treble’ 2008-2009.

Mafanikio hayo yalimfanya Guadiola kuwa ndiye kocha aliyefanikiwa kutwaa mataji mengi kwenye historia ya klabu hiyo hivyo kuna maelewano makubwa kati ya wawili hao na wafuatiliaji wengi wa masuala ya soka wanadhani siku moja Guardiola na Messi watakaungana tena kuipa mafaniko Man City.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Brexit Britain approved a European vaccine, German health minister says

Celebrating Britain's swift approval of BioNtech and Pfizer's coronavirus vaccine as a benefit of Brexit is misplaced since the...

Nairobi Expressway Turns Mombasa Rd into a ‘Parking Lot’ [VIDEO]

The ongoing Nairobi Expressway Project is expected to address the traffic jam issue in the city.  However, its construction phase...

Gardaí identify 28 people involved in PUP scheme fraud

Gardaí have identified 28 people engaging in identity and fraud offences to obtain money under the Pandemic Unemployment Payment...

Ukiukaji wa sheria kwenye uchaguzi wa Bosnia

Polisi wameendesha operesheni katika miji ya Srebrenica na Tuzla nchini Bosnia Herzegovina, kutokana na ukiukaji wa sheria ulioripotiwa kuwepo...

VIDEO | Lugo – Log in

https://www.youtube.com/watch?v=i6Mlklua3Aw ...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you