News Majaliwa, Ndugai na Mo Dewji kunogesha hafla ya kuwakaribisha...

Majaliwa, Ndugai na Mo Dewji kunogesha hafla ya kuwakaribisha Wabunge wapya tawi la Simba mjengoni Dodoma

-

Mwenyekiti wa tawi la Simba Bungeni almaarufu Simba mjengoni Mhe.Rashid Shangazi amesema kuwa tawi hilo limeanda hafla ya chakula cha usiku kesho kwa ajili ya kuwakaribisha wabunge wapya mashabiki wa Simba.

Mhe.Shangazi amesema kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ni miongoni mwa wageni wa heshima watakaohudhuria hafla ya kuwakaribisha wabunge wapya ambayo imeandaliaa na Wabunge wanachama wa Klabu ya Simba tawi la Bunge jijini Dodoma.

Hafla hiyo pia itahudhuriwa na Spika wa Bunge na Naibu Spika ambao ni wanachama wa Simba pamoja na mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Timu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Mhe.Shangazi amesema kuwa lengo la hafla hiyo itakayofanyika kesho jijini Dodoma ni kula chakula cha usiku pamoja, kufahamiana pamoja na wabunge wapya kupata fursa ya kujisajili kwenye tawi hilo na kujisajili na kadi ya uanachama ya Timu hiyo.

Shangazi amesema lengo la kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuuza bidhaa za klabu hiyo na kuwa wakala wa bidhaa na vifaa vya Simba pamoja na kupata sehemu mahususi ya wabunge kutazama mpira.

” Alichokisema Mwenyekiti Mo Dewji kuwa watanzani wengi ni Simba wala hakukosea, mfano hapa Bungeni wabunge wa zamani na wa sasa ambao wamejisajili Simba ni 280 unaweza ukaona namna gani tulivyo wengi.

Simba ni muongoza mwendo tutaeleza mipango kabambe tuliyonayo, lengo letu ni kulifanya tawi letu kuwa kubwa zaidi duniani, ni Bunge la Tanzania tu ambapo klabu ya mpira ina tawi ndani yake na klabu hiyo ni Simba pekee, wengine wakianzisha basi wamechukua kwetu,” Amesema Shangazi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Simba Bi.Barbara Gonzalez amesema kuwa timu   hiyo imejikita kuongeza ushindani  wa kimchezo barani Africa na Duniani.

Naye Meneja wa benki ya Equity Upendo Makula amesisitizia wabunge na  Wanachama ambao sio wanachama ni mashabiki tu waje Equity Bank wajisajili na  waweze kupata  kadi zao za uanachama.

Aidha amesema kuwa DOdoma wanaendelea vizuri na tayari wameshatoa kadi 1,000 hadi sasa.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Mr Price store in Carlow can sell groceries but not food, court rules

Dunnes Stores has secured a High Court injunction preventing a rival retailer from continuing to sell food products, but...

What Sonko’s Impeachment Means For Nairobi

The impeachment of Nairobi Governor Mike Sonko by the county assembly cast a shadow of uncertainty over the future...

Man Who Woke up in Morgue Dies

A man whose story broke the internet after he regained consciousness inside a morgue on Wednesday evening, November 25,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you