News Majitaka kupewa kipaumbele sekta ya maji

Majitaka kupewa kipaumbele sekta ya maji

-

Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameitaka Jumuiya ya Wasambazaji Maji Tanzania (ATAWAS) kutoa kipaumbele kwenye eneo la majitaka baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la usambazaji wa majisafi.

Mhandisi Kemikimba ametoa maelekezo hayo katika uzinduzi wa Kongamano la 8 la Maji katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper, jijini Dodoma.

“Kuna mafanikio makubwa kwa upande wa usambazaji maji, lakini kwa upande wa majitaka bado. ATAWAS mnatakiwa kuwekeza kiasi kikubwa kwenye eneo hili, ambapo lengo letu ni kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 kwa sababu majisafi ni mengi na itachangia kuwepo kwa majitaka mengi “, amezungumza Naibu Katibu Mkuu.

“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano ili kufanikisha azma hiyo, lakini pia ni lazima katika majadiliano yenu muweke msisitizo kwenye utafiti na ubunifu kwa kuwatumia Taasisi za Elimu ya Juu ili kuweza kupata suluhisho la kudumu litakalomaliza changamoto zote”, amesisitiza Mhandisi Kemikimba.

Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu ametoa wito kwa wadau wote wa Sekta ya Maji nchini kushirikiana na ATAWAS ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji kwa sababu peke yao hawatafanikiwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya ATAWAS na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA), Mhandisi Geofrey Hilly amesema ATAWAS imezindua rasmi mpango wa kuwajengea uwezo wanachama wake kwenye eneo la menejimenti ya rasilimali fedha, ukizingatia kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zinazozikabili Mamlaka za Maji na sekta kwa ujumla, ni usimamizi wa fedha za utekelezaji wa miradi mijini na vijijini.

Pia, ameongeza kuwa ATAWAS pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu zimeshasaini mkataba wa ushirikiano kwenye eneo la utafiti kwa lengo la kupata suluhisho la kudumu changamoto za kisekta.

Lengo la Kongamano hilo ni kujadiliana, kutathimini na kuzipatia ufumbuzi  changamoto za kisekta na kubaini fursa zilizopo ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kufikia  dira ya Taifa ya mwaka 2025, pamoja na lengo la sita (6) la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2030.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Advice against travel to the North likely under reopening plan

The government is strongly considering telling people not to travel to Northern Ireland from next week, due to the...

Ruto Watched Uhuru on TV During BBI Event – Spokesperson

Deputy President William Ruto's team has responded to his conspicuous absence at the BBI event at the Kenyatta International...

Baada ya kifo cha Maradona, Rais atangaza siku tatu za maombolezo

Rais wa Argentina Alberto Fernandez ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha gwiji wa nchi hiyo...

US looting oil, wealth of Syrian people: Iran UN envoy

Addressing a meeting of the UN Security Council on Syria, Majid Takht-Ravanchi said, " After almost 10 years of conflict, the...

Maisha ya nyota wa zamani wa Argentina Diego Maradona kwa picha

Umaarufu wake pekee haumtendei haki,. Diego Maradona alikuwa mchezaji mwerevu kupita kiasi katika uwanja wa mpira na mtu aliyezua...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you