News Mradi mkubwa wa maji Mugango-Kiabakari wasainiwa

Mradi mkubwa wa maji Mugango-Kiabakari wasainiwa

-

Wizara ya Maji imesaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi mkubwa wa maji wa Mugango- Kiabakari na kampuni ya UNIC CONSTRUCTION ENGINEERING (LESOTHO) ( PTY) LTD. ambao unatarajia kumalizika kwa muda wa miezi 24 na kuanza kuhudumia wananchi 200,000 kwenye vijiji 19 vilivyopo wilaya za Musoma na Butiama.

Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Athony Sanga amesema lazima Mradi huo uzingatie ubora na kuendana na thamani ya fedha Shilingi Bilioni .70.5 zilizotolewa na mfuko wa Badea na Soud Fund.

“Niombe Mkandarasi anayejenga Mradi huu aukamilishe kwa wakati, afanye kazi usiku na mchana Wananchi wa maeneo huska wanahitaji sana huduma ya Maji Safi na salama, Rais Katika ahadi yake alipokuja Mkoa wa Mara Kuomba kura alisema akichaguliwa tu lazima kazi ianze, na ameanza kutekeleza, itakuwa ni ajabu kuona Mkandarasi anasua sua na kushindwa kuukamilisha kwa muda uliopangwa kwenye mkataba wakati fedha zipo.”alisema Mh. Sanga.

Aliongeza kuwa, Mradi huo ukikamilika utaweza kutoa huduma ya Maji kwa Wananchi kwa miaka 20 kwa utoshelevu, ambapo pia utazalisha lita zaidi ya Mil.17 awamu ya kwanza kwa siku, huku uhitaji ukiwa ni lita Mil. 12 kwa siku na awamu ya pili utazalisha Lita zaidi ya Mil. 35 na baadhi ya vijiji vitaongezwa kwenye mradi na akasisitiza Mkandarasi kuzingatia ubora wa Mradi, muda wa kukamilika na thamani ya fedha zinazojenga Mradi huo.

Aidha Mh. Sanga alimtaka Mkandarasi huyo kuwapa nafasi za kazi Wananchi walioko maeneo ya Mradi waweze kuwajibika kuchimba mitaro na kazi nyingine zisizo za kitaalamu ikiwa Ni njia mojawapo ya kuwafanya wajipatie kipato kipindi chote cha Mradi huo sanjari na Viongozi wa maeneo huska wakitakiwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi kipindi chote Cha mradi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye baadhi ya vijiji vya jimbo lake vitanufaika na mradi huo Jumanne Sagini, alisema wakazi wa Butiama wataondokana na adha ya maji inayowakabili kwa sasa baada ya Mradi kukamilika.

“Ilikuwa ni aibu Sana Maji yanaenda mbali zaidi ya Km 400 mikoa ya mbali lakini Wananchi wa Butiama na Musoma wanakosa maji wakati wanazungukwa na ziwa Victoria , nimshukuru Sana Rais kwa uamzi wake wa kuleta Mradi huu haraka iwezekanavyo baada ya kuapishwa, hakika amejibu ombi na kilio cha Wananchi, niombe pia kata zinazopakana na Mto Mara ikiwemo kata ya Buswahili na Bukabwa ikiwezekana ziangaliwe nazo ziwekwe kwenye mradi awamu nyingine. Wananchi wapelekewe huduma ya maji” alisema Sagini.

Mkandarasi anayejenga mradi huo UNICK CONSTRUCTION ENGINEERING (LESOTHO) (PTY) LTD. He Yifeng/ Paul He amesema kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana aweze kukamilisha mradi huo kabla ya muda wa miezi 24, alisema anatambua dhamana aliyopewa ni kubwa Katika kuhakikisha Wananchi wanapata maji Safi na salama kwa ajili ya Maendeleo yao.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

MP proposes Iran’s withdrawal from NPT

The MP said Iran should give the Europeans six months to remove the sanction and if they could not...

Taulo za kike 1600 zakabidhiwa kwa wanafunzi Njombe

Na Amiri Kilagalilia,Njombe Mbunge wa viti maalumu mkoani Njombe Neema Mgaya amekabidhi msaada wa taulo za kike 1600 zenye thamani...

Mashabiki Simba wataka Mo Dewji akingiwe kifua

 Na Omary Mngindo, Kibaha TAWI Maarufu la Simba la Kibaha kwa-Mfipa Maarufu (Simba Tishio), limewataka viongozi wa matawi ya klabu...

IAEA: Iran’s top nuclear scientist stayed in shadows but his work was uncovered

Iranian scientist Mohsen Fakhrizadeh, who was killed on Friday, led a life of such secrecy that even his age...

Garissa University Terror Convict Commits Suicide in Prison

Garissa University terror attack suspect Rashid Mberesero reportedly committed suicide inside Kamiti Maximum Prison on Friday, November 27.  Details of the...

Oman condemns assassination of Iranian scientist

In a phone talk with his Iranian counterpart, Mohammad Javad Zarif, the Omani diplomat offered solemn condolence to the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you