News Msanii wa filamu Asha Boko aolewa kwa mara pili

Msanii wa filamu Asha Boko aolewa kwa mara pili

-

 

Msanii wa filamu wa muda mrefu hapa nchini Tanzania Asha Boko siku ya leo Novemba 20, ameweza kufunga ndoa kwa mara ya pili na mume wake Duwa Msafiri huko nyumbani kwao Mlandizi.

 Asha Boko amesema hakutaka ndoa yake ijulikane kwa sababu watu wangeweza kutia vizuizi isitokee na kesho watafanya sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo.

“Ni kweli nimeolewa leo nyumbani kwetu Mlandizi, mume wangu anaitwa Duwa Msafiri na kesho kutakuwa na sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo, nilikuwa sijatangaza kwa sababu nisingeolewa watu wangenitangaza ila taarifa nimetoa kwenye familia, ndugu, jamaa na marafiki, mume wangu sio mtu maarufu hawawezi kumuiba kwa sababu anajielewa” amesema Asha Boko

Asha Boko amefunga ndoa hiyo ikiwa ni mara yake ya pili baada ya mume wake wa kwanza kushambuliwa na majambazi hadi kufariki mwaka 2010 wakati walipovamiwa nyumbani kwao Kimara, Jijini Dar Es Salaam.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

US investigates potential bribery and lobbying schemes for pardons

The US Justice Department is investigating whether there was a secret scheme to lobby White House officials for a...

Barr appoints special counsel in Russia probe investigation

Attorney General William Barr has given extra protection to the prosecutor he appointed to investigate the origins of the...

US Covid death toll returns to grim early levels

Nearly 37,000 Americans died of Covid-19 in November, the most in any month since the early days of the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you