News Mtaturu apokelewa kwa kishindo jimboni kwake

Mtaturu apokelewa kwa kishindo jimboni kwake

-

Hivi ndivyo unaweza kusema kuwa ni Mafuriko ya wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Mbunge wao Mhe.Miraji Mtaturu walivyompokea kwa shangwe na furaha baada ya kuwasili katika Jimbo hilo la Singida Mashariki akitokea bungeni Dodoma kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumuani tena miaka mitano tena kwa ushindi wa kishindo. 

Akizungumza na baada ya kupokelewa na wananchi wake na Chama cha CCM Mhe.Mtaturu  amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kuendelea kumuamini  tena huku akisema kuwa atawatumikia wananchi bila kuwabagua kwa itikadi zao za kisiasa.


Aidha Mtaturu amewambia wananchi  kuwa uchaguzi kwasasa umekwisha hivyo wananchi washirikiane kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inapata mafanikio na yeye kama kiongozi wao atawatumikia wote bila ubaguzi.


“Tayari Mimi ni Mbunge wenu  nipo tayari kushirikiana nanyi, lakini pia tujenge mahusiano, tuachane na itikadi zetu za kisiasa sasa tujenge uchumi wa Jimbo la Ikungi, tumechelewa sana,”amesisitiza 


Hata hivyo Mhe.Mtaturu ametaja  vipaumbele saba atakavyoanza navyo ikiwemo suala la elimu ambapo atasimamia kuhakikisha watoto wanapata elimu bora,Maji,Umeme,Afya pamoja na miradi iliyopo inatekelezwa na kuibua mingine.


Aidha Mhe.Mtaturu amewahamasisha akinababa kuunda vikundi vya wakulima ili waweze kupata mikopo itakayosaidia kuinua kilimo chao katika wilaya ya Ikungi na pia wataweza kupata mikopo wakiunda vikundi hivyo.


Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Somalia Expels Kenyan Ambassador Over Polls Interference

Somalia has expelled the Kenyan Ambassador to Mogadishu, Retired Major General Lucas Tambo and has recalled its own diplomat...

Nchelenge Man Murders Daughter in Custody Dispute with Ex-Wife

A 22-year-old man has murdered his one-year daughter following a custody dispute...

Kenya Power Bows to Public Outcry Over Bills

Kenya Power has resumed issuing a breakdown of the pre-paid electricity tokens after previously putting a stop to sending detailed...

Iran’s petchem production capacity increases by 10mn tons

By implementing a number of six petrochemical projects since the beginning of the current year, the country’s petrochemical production...

Crunch Brexit talks resume in London for what could be final week

Crunch talks aimed at securing a post-Brexit trade deal between the European Union and UK will resume today in...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you