News Mwinyi awataka Mawaziri wapya Zanzibar kuyafanyia kazi mambo 13

Mwinyi awataka Mawaziri wapya Zanzibar kuyafanyia kazi mambo 13

-

 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Mawaziri kuyafanyia kazi mambo kumi na tatu ili kuleta ufanisi Serikalini.

1. Kila waziri aijue wizara na Taasisi zake kwa kuzitembelea.

2. Kila Waziri atengeneze Mpango kazi na Bajeti kwa kutumia ilani, hotuba ya Rais, ahadi za kampeni, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar na kupata maoni ya Wadau wa wizara.

3. Kutembelea miradi yote ya wizara kwa kuangalia ubora, utaratibu wa zabuni, malipo yaliyofanyika na muda wa kumaliza.

4. Uwajibikaji wa Watendaji. Kila mtu awajibike kwa kazi aliyopewa na Huduma zitolewe kama  zinavyotakiwa. 

5. Kuhakikisha  haki za watu zinatolewa, Wafanyakazi walipwe posho zao fedha za safari overtime walipwe pale wanapostahiki, haki za wananchi zitolewe na Watu wasikilizwe .

6. Utawala bora, Rushwa ubadhirifu uondolewe, Wizi wa makusanyo na fedha za bajeti na Matumizi mabaya ya  Fedha za miradi.

7. Ukusanyaji wa mapato ya Serikali  ZRB na TRA ziangaliwe. 

8. Ubunifu; kila mtu abuni mambo mapya katika kazi, asisuubiri kuelekezwa, Tumia wataalamu waliopo kuleta ubunifu. 

9. Urasimu uondoe usumbufu katika kupata huduma, Njoo kesho njoo kesho iondoke, Wananchi wapate majibu na mambo yenye maslahi ya Umma yasicheleweshwe. 

10. Mawaziri wawe wepesi wa kuleta mapendekezo ya sheria pale ambapo sheria ni kikwazo.

11. Taarifa  zinazofanywa zitolewe kwenye vyombo vya habari na mawaziri wawe marafiki na waandishi wa habari.

12.Wasikilize malalamiko ya watu. Kila wizara iwe na utaratibu wa kusikiliza malalamiko ya watu na kutumia  teknolojia kutekeleza hili kama vile mitandao ya kijamii.

13. Kuhakikisha maeneo ya kufanyia kazi yanakuwa katika Mazingira mazuri ya kufanyia kazi, Mji wetu ni mchafu hakuna hata sehemu moja ambayo tunasema hapa afadhali, itafutwe njia mbadala ya kubafilisha hali hii.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

What Sonko’s Impeachment Means For Nairobi

The impeachment of Nairobi Governor Mike Sonko by the county assembly cast a shadow of uncertainty over the future...

Performers protest outside Leinster House amid ongoing closures

Performers, including dancers, actors and singers have gathered outside Leinster House protesting against the ongoing closure of the performing...

China’s lunar probe begins journey home with cargo of samples

China’s lunar probe has lifted off from the moon with a cargo of lunar samples on the first stage...

Turkey military exports to Azerbaijan up 600% this year

Turkish military exports to Azerbaijan increased by a staggering 610 per cent over the course of 2020, according to...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you