News Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar aachiwa na Polisi

Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar aachiwa na Polisi

-

 Jeshi la Polisi kisiwani Zanzibar leo Jumanne Novemba 17, 2020 limemuachia naibu katibu mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar,  Nassor Ahmed Mazrui aliyekamatwa mjini Unguja Oktoba 28, 2020 na watu wengine 32.

Mbali na Mazuri, taarifa zilizoifikia Mwananchi Digital zinaeleza kuwa aliyekuwa  kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ayoub Khamis Bakari naye ameachiwa.

Tangu Alipokamatwa viongozi wa chama hicho walitoa matamko mbalimbali wakitaka aachiwe kwa dhamana au kupelekwa mahakamani ikiwa ni baada ya baadhi kuachiwa huku kiongozi huyo akiendelea kushikiliwa.

Alipoulizwa kuhusu kuachiwa kwa wawili hao kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadhi Haji Hassan  amesema licha ya kuwepo kwa taarifa hizo hawezi kuzithibitisha.

Amebainisha kuwa viongozi wa ACT kesi yao ilikua chini ya makao makuu ya jeshi hilo Ziwani mjini Unguja.

‘’Ni vyema mkamsikiliza kamishna wa polisi Zanzibar  yeye ndio atakua na maelezo mazuri kuhusu taarifa hizo, “ amesema Haji.

Kamishna wa jeshi hilo Zanzibar, Mohamed Haji Hassan ameieleza Mwananchi Digital kuwa anafuatilia kwa kina taarifa hizo na baadaye atatoa maelezo kwa kina.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo mwanasheria mkuu wa chama hicho, Omar Sidi Shabani amesema wawili hao wameachiwa leo jioni.

Amesema anafuatilia kujua masharti zaidi ya kuachiwa kwao na kwamba baada ya hapo chama hicho kitatoa taarifa rasmi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Gaiety Theatre to auction off projectors next week

The Gaiety Theatre is set to auction off two projectors next week, according to the Irish Times. The pair of...

Pompeo says Iran ‘desperately’ keen to return to talks for sanctions relief

US Secretary of State Mike Pompeo on Friday said Iran was "desperately" signaling its willingness to return to the...

Three men charged in Offaly over crime and anti-social behaviour

Three men have been charged as part of a crackdown on crime and anti-social behaviour in Co Offaly. They were...

UK and EU fail to reach deal as trade talks paused

UK and the European Union failed on Friday to secure a trade agreement, saying talks would be paused so...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you