News Rais Dk.Hussein Mwinyi atembelea Wafanyabiashara

Rais Dk.Hussein Mwinyi atembelea Wafanyabiashara

-

 

RAIS  wa Zanzibar na Mwenywkiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameutaka uongozi wa Serikali ya mkoa wa Mjini , Baraza la Manispaa na wafanyabiashara wa Kijangwani kukaa Pamoja na kutafuta sehemu ya kudumu itakayokuwa nzuri kwa wafanyabiashara ili kuweza kufanya biashara zao kwa urahisi.

Akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo wa kijangwani, Baada ya wafanyabiashara hao kutakiwa kuhama sehemu hiyo na mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuhamia Katika soko la Jitimai, jambo ambalo wafanyabiashara hao hawajakubaliana nao kutokana na eneo hilo si rafiki kwao.

Alisema kuwa kukaa pamoja kitasaidia kutafuta sehemu iliyokuwa nzuri ikiwemo miundombinu bora ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kufanyabiashara vizuri.

Alisema wote wanafahamu soko hilo si la kudumu na lipo kwa muda na kuwataka kipindi hichi cha kutafuta eneo jengine kubaki hapo hapo hadi sehemu itakapopatikana.

“Soko hilo litakuwa la muda vile vile maana soko la kudumu litachukua fuda vile vile hivyo wafanyabiashara wabaki walipo” alisema.

Aidha alisema Ilani ya Chama cha Mapinduzi imesema kuwa itatekeleza mazingira bora ya wafanyabiashara na kuwapa vitambulisho ili kodi zisitolewe kila siku, hivyo alisema kuwa ahadi aliyoitoa ipo pale pale kwa kuona mazingira yanakuwa mazuri ya kufanyabiashara.

“Nakuahidini nitakuwa wa kwanza kulisimamia suala hili kwani nimeahidi na nimekuja hapa nitakuwa wa kwanza kulisimamia hili” alisema.

Akizungumzia mradi wa kituo cha mabasi ya kufikia na kuondoka na soko, alisema mradi huo unalengo la kuwawekea mazingira mazuri ya biashara, hivyo wafanyabiashara hao hawana budi kukubaliana nao ili kuona mazingira mazuri yanakuwepo Katika ufanyaji wa biashara.

Hivyo, aliwasisitiza kuharakisha utafutaji wa eneo kwa wafanyabiashara ili mradi ukiokusudiwa kuweza kufanya kazi kea wakati uliopangwa.

“Muharakishe kutafuta hilo soko la muda kama hamuwezi kukipata mimi nitalipata” alisema.

Sambamba na hao, aliwataka viongozi hao kufika Ofisini kwake kwa kumpatia maelezo ya kina ya kitu ambacho kinataiwa kufanyika katika soko la Kijangwani pamoja na maelezo waliyokubaliana na wafanyabiashara kuhusu soko la muda.

Sambamba na hayo, Dk.Mwinyi alisema kuwa Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwa na mji safi Kila sehemu hivyo wafanyabiashara hao kuendeleza usafi wa mji.

“Hakutokuwa na tatizo mazungumzo niliyoyaelekeza yaanze mara moja na nimewasisitiza waje ili tujue mradi huu unaanza lini na wapi kwani nitasimamia mimi mwenyewe” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Khatib, alisema kuwa uamuzi wa kuondoshwa wafanyabiashara hao upo katika mpango wa serikali ambao sehemu hiyo inataka kujegwa soko kubwa pamoja sehemu ya kituo cha kufikia daladala na kuondokea.

Nao Wafanyabiashara hao akitoa malalamiko hayo mbele ya Rais, walisema kuwa kuhamama kwao kunasababishia mitaji yao kufa na biashara kutoendelea.

“Hatukatai kuhama katika soko hili ila tunaomba tutafutiwe sehemu iliyokuwa nzuri maana kuhama hama huku kunatuadhiri sana” walisema.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Vaccine will ‘motivate’ people into following Covid-19 rules

Taoiseach Micheal Martin said the imminent arrival of a coronavirus vaccine will “motivate” people into following pandemic health rules. Rejecting...

Zitambue mbinu za mafanikio katika kilimo

1. Zalisha kwa wingi.Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama...

Jifunze kuzalisha malisho ya wanyama kwa njia ya kitaalamu “hydroponic fodder”

Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalikaHYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya kuotesha mazao bora yenye tija...

IAEA shall ensure confidentiality of safeguards information

In a Friday tweet, Kazem Gharibabadi wrote, "@iaeaorg confidential report, based on Iran's confidential letter, appeared in Media immediately even...

Breakthrough to resolve Gulf crisis, UAE remains hesitant

Qatar's Foreign Affairs Minister, Mohammed Abdur Rahman Al-Thani, said Friday that the solution to the Gulf crisis must be...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you