News RC Ayoub awapa neno wanafunzi wa Umoja Uzini

RC Ayoub awapa neno wanafunzi wa Umoja Uzini

-

 

Mkuu wa Mkoa kusini unguja bwana,  Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka wanafunzi wa skuli ya Umoja Uzini kujiandalia mazingira yao ya baadae kwa kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani yao wa kidatu cha nne inayotarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.

Ameyasema wakati akizungumza na wanafunzi hao wanaojiandaa kufanya mitihani yao ya taifa  mwaka huu huko katika skuli ya Umoja Uzini amesema kuwa elimu ndio dira ya maisha ya kila mwanafunzi hivyo ni vyema wakujitahidi kwa bidi ili waweze kufikia malengo yao walio jiwekea ya kielimu. 

Bwana, Ayoub amewapongeza wanafunzi hao kwa kuonyesha ari na bidii kwa kutumia muda wao katika kujisomea masomo ya ziada hali ambayo inakwenda sambamba na azma ya serikali ya mkoa huo ya kuengeza idadi ya ufaulu wa daraja la kwanza na kutokomeza wimbi la wanafunzi wanaopata zero.

Aidha amesema kuwa serekali itaendelea na jitihada zake za kuandaa mazingira bora ya elimu ikiwemo kujenga skuli za kisasa pamoja na vifaa vya masomo ya sayansi ili kuweza kutowa wataalamu watakao weza kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali katika kijamii. 

Katika hatua hiyo  amewaagiza watendaji wa wilaya ya kati kutatuwa changamoto zinazo wakabili wanafunzi hao kwa haraka kwa lengo la kuwafanya waweze kusoma katika mazingira yalio bora ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu. 

kwa upande wake mwalimu Mkuu wa skuli ya Umoja uzini amesema lengo la kuazisha kambi kwa watahiniwa hao ni kuwapatia muda wa kutosha kupitia masomo yao ambapo amesema kuwa wamejipanga kikamilifu ili kuona skuli yao inafanya vyema katika mtihani wa taifa kwa kufaulisha wanafunzi wengi.

Nao wanafunzi wa skuli ya uzini wamemuahidi Mkuu wa mkoa huyo kwamba watahakikisha wanasoma kwa bidii ili kuweza kufanya vyema katika mitihani yao inayowakabili huku wakieleza kuwa watafanya mitihani hiyo bila ya kufanya udanganyifu wowote ule katika kipindi chote cha mitihani yao.

Katika maelezo yao wanafunzi hao walisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama na kukatikakatika  kwa umeme katika eneo lao pamoja na upungufu wa chakula.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

California certifies election results to clear Joe Biden’s path to White House

California has certified its presidential election and appointed 55 electors pledged to vote for Joe Biden, officially handing him...

Kilimo bora cha mahindi

KANUNI YA KWANZAPanda mapemaTayarisha shamba mapema kwa zana yoyote iliyo ndani ya uwezo wako (jembe, maksai, trekta).Kwa wilaya ya...

UK rights groups decry France’s anti-Muslim drive

British advocacy groups have condemned France's decision to shut down anti-racism group Collective Against Islamophobia in France (CCIF), Anadolu Agency reports. While...

Sinn Féin member resigns after being confronted over critical tweets

A Sinn Féin member has resigned from the party saying she was told not to discuss internal issues in...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you