News RC Tabora awataka walimu kuwaandaa vijana kuwa wazalendo watakaoleta...

RC Tabora awataka walimu kuwaandaa vijana kuwa wazalendo watakaoleta maendeleo ya kweli ya Taifa

-

WALIMU Mkoani Tabora wametakiwa kushirikiana na jamii ili kuwajenga vijana katika misingi ya uzalendo wa kweli ambao utawafanya kuipenda nchi yao na kuwa tayari kuleta maendeleo ya kweli kwa kutumia akili na vipaji vyao.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati wakati wa uzinduzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Arba Light iliyopo Manispaa ya Tabora.

“Jitahidini kuwaandaa wanafunzi kuwa wazalendo ambao watakuwa na uchungu na nchi yao na hawako tayari kuwa vibaraka wa watu mengine ” alisema.

Aliongeza wanafunzi watakiwa kuwajenga katika nidhamu na weledi ambao utawafanya kuwa tayari kufanya kazi kwa moyo wao wote kwa ajili ya kuipeleka nchi mbele.

“Hatutarajii miongoni mwa wanafunzi mnaowafundishi tupate vibaraka wanaotumika kuiharibu nchi yetu na mkoa wetu wa Tabora…hatutarajii tupate vijana kutokana na hao watakaokuwa chanzo cha mitafaruku hapa nchini” alisema

Dkt. Sengati alisema vijana wanatakiwa kulelewa toka awali katika misingi ya uzalendo halisi wa Kitanzania ambao wako tayari kutetea misingi ya kijamaa iliyojengwa toka uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hadi uongozi wa sasa wa Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli kwa kuwatetea wanyonge.

“Tuendelee kuwalea vijana katika misingi mizuri…hakuna rasilimali muhimu kama binadamu , ukikosea katika malezi ya vijana toka awali , ukikosea katika elimu ya vijana utatengeneza kijana asiyekuwa na misingi ya utaifa…kijana asiyekuwa na misingi ya uzalendo na asiyeelewa kuwa hana nchi nyingine zaidi ya Tanzania na tutakuwa tumepoteza mwelekeo wao” alisema.

Dkt. Sengati alisema ni lazima walimu na jamii waendelee kutengeza vijana ambao watatumia akili na vipaji vyao katika kuhakikisha wanaliendeleza na kulitetea Taifa lao.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameagiza Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) na Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) mkoani humo kuhakikisha wanapeleka huduma katika Taasisi mbalimbali ikiwemo shule ya Arba Light ambayo haina umeme na hakuna barabara za uhakika.

Alisema hatua hiyo itasaidia wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kufika shule pasipo vikwazo ili hatimaye waje kuwa watumishi na wataalamu ambao watasaidia kuendeleza nchi na Mkoa wa Tabora

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Kavindele Toll Plaza Rakes K1.5 Million per Month

The National Road Fund Agency says it is now collecting over 1.5...

UK says aware of attack on vessel off Yemen coast: Report

The authority later updated the advisory notice on its website to say the “incident is now complete. Vessel and...

CHANGAMKIA: VIWANJA VINAUZWA BEI YA KUTUPWA, VIWNJA VIPO DAR VIKINDU

Basi Ondoa shaka SUYUTWI LINK TANZANIA, Tumeandaa mradi mkubwa wa wanne(4) wenye wenye viwanja zaidi ya 300, Mradi wetu...

AUDIO | udoudo – Mama | Download

Download | udoudo...

Maraga Retires in Special Town Away From Nairobi

Chief Justice David Maraga has announced his retirement plans ahead of proceeding to terminal leave on Friday, December 11, 2020.  CJ...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you