News Serikali ya Ethiopia yatangaza kuendeleza operesheni dhidi ya TPLF

Serikali ya Ethiopia yatangaza kuendeleza operesheni dhidi ya TPLF

-

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ametangaza kuwa operesheni ya kijeshi dhidi ya vikosi vya waasi vya Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo imefikia hatua za mwisho.

Katika taarifa aliyotoa kupitia akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Ahmed alisema kuwa mudai wa siku 3 uliopewa vikosi vya TPLF vinavyoongoza jimbo la Tigray umekwisha, na operesheni hiyo itaendelea hadi hatua ya mwisho.

Akiwashukuru wanamgambo waliojisalimisha kwa jeshi la kitaifa la Ethiopia, Ahmed alibainisha kutokana na uamuzi wa kujisalimisha, watu hao wameweza kuokoa maisha yao kwa kuwajibika na kutii sheria.

Kwa upande mwingine, Mwanasheria Mkuu wa Ethiopia alitangaza kuwa akaunti za benki za kampuni 34 zinazohusiana na TPLF zimezuiwa.

Kikosi cha anga cha Ethiopia kiliendesha shambulizi la anga katika mji wa Mekelle ambao ni mji mkuu wa jimbo la Tigray hapo jana, kuwa kujibu mashambulizi ya roketi ya TPLF yaliyotekelezwa Amhara na Eritrea.

Waziri Mkuu Ahmed aliwahi kuzungumza kwenye televisheni ya kitaifa wiki iliyopita na kutoa wito wa kujisalimisha kwa vikosi vya TPLF.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Journalist Who Left TV Job to Save Lives

James Murimi Nyambura is a man on a mission, using the challenges he encountered growing up, to give hope to those...

US, Zionists play a key role in assassination of Fakhrizadeh

TEHRAN, Dec. 05 (MNA) – Consul General of Yemeni Embassy in the Islamic Republic of Iran said that the...

Peace protesters form human chain outside German parliament

Hundreds of peace protesters have formed a human chain outside Germany’s parliament, calling for disarmament and an end to...

Church housing New York’s Liberty Bell gutted by fire

A historic church in lower Manhattan that houses New York’s Liberty Bell and whose congregation dates to the city’s...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you