News Taifa Stars yagawa pointi na Tunisia, yafungana 1-1

Taifa Stars yagawa pointi na Tunisia, yafungana 1-1

-

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo Novemba 18 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki Afcon.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni muhimu kwa Stars kushinda kwa kuwa ule wa kwanza ugenini ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 nchini Tunisia ulikuwa mgumu kwa Stars kwa kuwa walikubali kufungwa kipindi cha kwanza.

Zikiwa zimetofautiana dakika nane kwa kuwa mchezo wa kwanza Stars ilifungwa bao la ushindi dakika ya 18 leo Uwanja wa Mkapa imefungwa dakika ya 10.

Bao la kuongoza kwa Tunisia ambao tayari wameshafuzu michuano ya Afcon lilipachikwa kimiani na Saif Eddine Khaoul.

Iliwalazimu Stars kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja huku safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na nahodha John Bocco ikiwa haijafanya jaribio la hatari ndani ya dakika 45.

Bao la kuweka usawa na kuipa pointi moja Stars lilifungwa na Fei Toto ambaye alianzia benchi na alichukua nafasi ya Himid Mao dakika ya 47 kwa shuti kali akimaliza pasi iliyotengwa na Bocco

Pointi hiyo moja inaifanya Stars iwe nafasi ya nne ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi nne huku Tunisia ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 10.

Nafasi ya nne ipo mikononi mwa Libya yenye pointi tatu na ile ya pili ni mali ya Equatorial Guinea yenye pointi 6 kwenye kundi J.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

UAE suspends issuing visas to citizens of 13 Muslim majority countries

The United Arab Emirates (UAE) has suspended issuing travel and work visas for citizens of 13 mostly Muslim-majority countries,...

Huu hapa wasifu wa Diego Armando Maradona

 Mmoja wa wachezaji waliobarikiwa, Argentina ilijivunia kipaji cha kipekee, madoido ya ajabu akiwa uwanjani, maono na kasi vilivyovutia mashabiki...

VIDEO | Meja Kunta – Chura Superstar

https://www.youtube.com/watch?v=sdwSLp9h7Dk ...

Ifahamu historia ya gwiji wa soka duniani, Diego Maradona kiundani

Mmoja wa wachezaji waliobarikiwa, Argentina ilijivunia kipaji cha kipekee, madoido ya ajabu akiwa uwanjani, maono na kasi vilivyovutia mashabiki...

Man Found Alive in Mortuary Speaks After 3-Hour Ordeal

Peter Kiplangat Kigen, the man who regained consciousness while in a mortuary in Kapkatet Hospital, Kericho County shared details after...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you