News TBS yateketeza vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani zaidi...

TBS yateketeza vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani zaidi ya milioni 125

-

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza vipodozi  vyenye viambata sumu vya thamani ya Shilingi milioni 125 baada ya  kufanyika kwa ukaguzi wa kushitukiza kwenye maghala ya kuhifadhia vipodozi ambayo hayajasajiliwa.

Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku vilikutwa katika maghala la kampuni ya Kimario Cosmetics  hivi karibuni na wakaguzi wa TBS jijinii Arusha na kukamatwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2019.

Mmiliki wa ghala hilo Pamphil L. Kimario amelipa shilingi milioni 3.5 ikiwa ni gharama ya kuteketeza  bidhaa hizo hatarishi kwa afya ya binadamu kwani zinapotumiwa huweza kusababisha madhara mbambali kwa mtumiaji,

Baadhi wa Watanzania wamekuwa wakitumia vipodozi hivyo vyenye viambata vya sumu ambavyo vina kemikali ya Mercury na Hydoroquinone kwa lengo la kung’arisha  ngozi zao na hata kubadili rangi ya ngozi hizo bila kujali madhara yatokanayo na bidhaa hizo.

Vipodozi vyenye kemikali ya Mercury kwa Mujibu ripoti ya Shirika la Afya Duniani(WHO) ya mwaka 2020, vikitumika kwa muda mrefu vinasababisha magonjwa ya figo, mapafu, ngozi, macho mfumo wa fahamu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na mfumo  wa kinga ya mwili na kwa upande wa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha magonjwa ya kansa ya ngozi.

Sheria ya Fedha  Na. 8 ya mwaka 2019 iliipa Mamlaka TBS  ya kusimamia usajili wa bidhaa za chakula ,vipodozi , maghala ya kuhifadhia chakula na vipodozi pamoja na migahawa na mahoteli jukumu  lillilokuwa likifanywa hapo awali na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa Chakula na Vipodozi (TFDA).

Utekelezaji wa Sheria hiyo ya Fedha ulianza rasmi tangu Julai 2019, hivyo kuwalazimu wauzaji wazalishaji  na wauzaji wa vipodozi kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ya kuhifadhia.

Shirika pia limeteketeza bidhaa nyingine zisizofaa za vipodozi na vyakula  zilizokamatwa katika kaguzi zilizofanyika nyakati tofauti katika maeneo mengine Arusha na nje ya Arusha  katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2020.  

TBS inaendelea na ukaguzi huu nchi nzima  pamoja na kuwahimiza wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zilizopo kwa kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala  ili kuepuka usumbufu. Pia wauzaji wa vipodozi wanahimizwa kuwa na orodha ya bidhaa za vipodozi visivyoruhusiwa ambayo inapatikana katika tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

California certifies election results to clear Joe Biden’s path to White House

California has certified its presidential election and appointed 55 electors pledged to vote for Joe Biden, officially handing him...

Kilimo bora cha mahindi

KANUNI YA KWANZAPanda mapemaTayarisha shamba mapema kwa zana yoyote iliyo ndani ya uwezo wako (jembe, maksai, trekta).Kwa wilaya ya...

UK rights groups decry France’s anti-Muslim drive

British advocacy groups have condemned France's decision to shut down anti-racism group Collective Against Islamophobia in France (CCIF), Anadolu Agency reports. While...

Sinn Féin member resigns after being confronted over critical tweets

A Sinn Féin member has resigned from the party saying she was told not to discuss internal issues in...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you