News Trump awauliza washauri wake uwezekano wa kuzishambulia Iran

Trump awauliza washauri wake uwezekano wa kuzishambulia Iran

-

Rais wa Marekani, Donald Trump aliwauliza wasaidizi wake kuhusu uwezekano wa kuvishambulia vinu vya nyuklia vya Iran, miezi miwili kabla hajaondoka madarakani. Taarifa hizo zimeripotiwa jana na gazeti la New York Times. 

Kwa mujibu wa gazeti hilo, wasaidizi wa ngazi ya juu wa Trump walimshauri kutofanya mashambulizi, wakimueleza kwamba hatua hiyo inaweza kusambaa na kuwa mzozo mkubwa katika wiki zake za mwisho za urais. 

Mkutano huo uliofanyika siku ya Alhamisi katika Ikulu ya Marekani, ulitokana na taarifa za Shirika la Kimataifa la kudhibiti matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA kwamba Iran imeongeza kurutubisha madini ya uranium mara 12 zaidi ya kiwango ambacho kinaruhusiwa katika makubaliano na mataifa makubwa yenye nguvu. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, Kaimu Waziri wa Ulinzi Christopher Miller na Mwenyekiti wa baraza la kijeshi, Mark Milley.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Iran holds funeral for military nuclear scientist

Iran has held a funeral service for the scientist who founded its military nuclear programme two decades ago. The Islamic...

Houthis claim killing of 8 Saudi soldiers in Marib

Yemen's Houthi rebel group has claimed the killing of eight Saudi soldiers in eastern Yemen, Anadolu reports. "The missile force...

Trump senior aide Kushner and team heading to Saudi Arabia, Qatar

White House senior adviser Jared Kushner and his team are headed to Saudi Arabia and Qatar this week for...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you