News Twaha Kiduku: Mwakinyo ni bondia bora ila asije akalewa...

Twaha Kiduku: Mwakinyo ni bondia bora ila asije akalewa sifa

-

 

Bondia Twaha Kiduku ameeleza kuukubali uwezo wa Hassan Mwakinyo na kumtaja kuwa ni bondia bora ila akamtahadharisha asije akalewa sifa kwa mafanikio anayopitia sasa ulingoni.

Twaha bondia namba mbili kwa ubora nchini kwenye uzani wa super welter nyuma ya Mwakinyo amempongeza mpinzani wake huyo kwa uwezo aliouonyesha hivi karibuni alipotetea ubingwa wa Mabara wa WBF kwa ushindi wa TKO dhidi ya Jose Carlos Paz wa Argentina.

“Ni pambano ambalo Mwakinyo alicheza vizuri mno, kuanzia raundi ya kwanza hadi ya nne aliposhinda. Nilikuwa ukumbini na kushuhudia na nilikwenda kumpongeza kwa namna alivyocheza.

“Nilitamani kumpa ushauri huu, lakini mazingira hayakuwa rafiki pale, nimsisitize tu mdogo wangu na bondia mwenzangu kuendelea kukaza afanye vizuri zaidi ya anavyofanya sasa. Isije ikatokea akalewa sifa atapotea,” alisema #Twaha anayemzidi Mwakinyo miaka mitatu akiwaambia Waandishi wa Habari.

Akaongeza, “Mwakinyo namuamini hana masihara na mazoezi, ninachoweza kumwambia aendelee kukaza hivyo hivyo ili azidi kufanya vizuri na kuitangaza ‘boxing’ ya Tanzania kimataifa kama walivyofanya waliomtangulia na mabondia wengine wanaopigana sasa nikiwamo mimi,” amesema.

Kuhusu kuwa na ndoto za kuzichapa na bondia huyo, #Kiduku amesisitiza kuwa bado mpango huo upo na unacheleweshwa na #Mwakinyo mwenyewe.

“Natamani itokee akubali kupigana na mimi, ila naamini ipo siku itatokea tu na pambano kati yangu na Mwakinyo litapigwa,” amesisitiza.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Turkey slams France’s call for Nagorno-Karabakh independence

The French Senate's adoption of a resolution urging the government to recognise Nagorno-Karabakh as an independent republic is "ridiculous, biased...

Too many people using homelessness services are dying, Varadkar says

Too many people using homelessness services are dying prematurely in Ireland, the Tánaiste has said. The number of deaths appears...

Lebanon ‘drug dealer’ arrested in Brazil

A Lebanese-Brazilian man was arrested in Sao Paolo on Monday on drug trafficking charges, the New Arab reports. Assad Khalil Kiwan...

Government acted appropriately during Woulfe process, Justice Minister says

The Government acted “appropriately” throughout the Seamus Woulfe appointment process, Justice Minister Helen McEntee has said. The need to ensure...

Biden’s Cabinet likely to get US mired in more wars

On Tuesday, Biden announced his selection of Antony Blinken as secretary of state, Jake Sullivan as the national security...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you