News Viongozi wa Al- Shabaab wapigwa marufuku kuingia Marekani

Viongozi wa Al- Shabaab wapigwa marufuku kuingia Marekani

-

Marekani imewawekea vikwazo viongozi wawili waandamizi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab waliohusika na utekelezaji wa shambulio la kigaidi katika kambi ya jeshi nchini Kenya.

Afisa mmoja wa jeshi la Marekani na wanakandarasi wawili waliuawa mnamo mwezi Januari katika shambulio lililtokea kambi ya Simba kisiwa cha Manda.

Hilo lilikuwa shambulio la kwanza kutekelezwa na kundi la Al-Shabab dhidi ya jeshi la Marekani nchini Kenya.

Wizara wa Mambo ya Nje Marekani imesema kuwa imewatambua Abdullahi Osman Mohamed na Maalim Ayman katika orodha ya magaidi wa kimataifa.

Taarifa kutoka wizara hiyo imesema Bwana Mohamed ni mtaalamu mwandamizi wa vilipuzi wa kundi la Al-Shabab na kiongozi wa mausala yao ya mawasiliano huku Bwana Ayman akihusishwa na kupanga shambulizi lililotokea katika kambi ya Simba.

“Raia wa Marekani wamepigwa marufuku kujihusisha na shughuli za muamala za aina yoyote na Mohamed and Ayman. Mali zao nchini Marekani zimezuiwa,” Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Junior Minister calls for panel increases for All-Ireland finals

The Minister for State for Skills and Further Education is calling for the All-Ireland final panel sizes to be...

Funeral ceremony of martyr ‘Mohsen Fakhrizadeh’ starts at MoD

The ceremony was attended by the Chief of General Staff of Iranian Armed Forces Major General Mohammad Hossein Bagheri,...

Afghanistan condemns Fakhrizadeh’s assassination

In a message condemning the assassination of the prominent Iranian nuclear scientist Mohsen Fakhrizadeh, the Afghan Foreign Ministry expressed...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you