News Waandamanaji zaidi ya 700 wakamatwa na polisi kwenye maandamano...

Waandamanaji zaidi ya 700 wakamatwa na polisi kwenye maandamano ya kuipinga serikali ya Belarus

-

Zaidi ya watu 700 wameripotiwa kutiwa mbaroni na vikosi vya usalama kwenye maandamano yaliyofanyika hapo jana kwa ajili ya kupinda serikali ya utawala nchini Belarus.

Msemaji kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Olga Chemodanova, alitoa maelezo kupitia mtandao wa kijamii na kuarifu kufanyika kwa maandamano kinyume cha sheria katika maeneo 35 kote nchini.

Chemodanova aliarifu kuwa maandamano hayo yameanza kupungua huku maafisa wa polisi wakichukua tahadhari zinazohitajika kuhakikisha hali ya utulivu na usalama inaimarika.

Akibainisha waandamanaji walionyesha hali ya kuzusha vurugu katika mji mkuu wa Minsk, Chemodanova alisema kuwa waandamanaji walifunga baadhi ya barabara na kuzuia magari na raia kupita.

Chemodanova aliongezea kusema kuwa waandamanaji hao walilazimika kukamatwa baada ya kukaidi agizo la kusitisha maandamano na tahadhari zilizotolewa na polisi.

Chemodanova pia alibainisha kuwa zaidi ya watu 250 walishiriki kwenye maandamano katika miji ya Brest na Grodno bila idhini, na kusema,

“Zaidi ya watu 700 waliokiuka sheria walikamatwa kwenye maandamano kote nchini na wataendelea kuwekwa chini ya ulinzi hadi watakapofikishwa mahakamani.”

Baada ya Rais wa sasa Alexander Lukashenko kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika Belarusi mnamo Agosti 9, maandamano yalianza dhidi yake kwa madai kwamba “uchaguzi haukutendeka kwa haki.”

Waandamanaji wamekuwa wakiandamana kila wikendi nchini humo na kumtaka Rais Lukashenko aachie madaraka.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Iran holds funeral for military nuclear scientist

Iran has held a funeral service for the scientist who founded its military nuclear programme two decades ago. The Islamic...

Trump senior aide Kushner and team heading to Saudi Arabia, Qatar

White House senior adviser Jared Kushner and his team are headed to Saudi Arabia and Qatar this week for...

Iranian researcher finds reason of disorders in space travels

The results of examining astronauts in space have shown that space travels increase the likelihood of astronauts becoming ill outside the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you