News "Wanaume wa Mbeya wanapenda kulelewa"- Chalamila

“Wanaume wa Mbeya wanapenda kulelewa”- Chalamila

-

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa mkoa wa Mbeya, wameachiwa jukumu la kuendesha familia zao huku wanaume wakiongoza kufanya vitendo vya dhuluma dhidi ya mali zinazotafutwa na wake zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la sita la jinsia ngazi ya wilaya, ambalo limefanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

RC Chalamila amesema kuwa wanawake wengi mkoani humo, ndiyo wanaobeba majukumu ya kutunza na kulea familia, ambapo hufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kuuza mboga na matunda, wakati wanaume wakitumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni  pamoja na kunyang’anya fedha wanazopata kwenye biashara na kwenda kuhonga michepuko.

“Idadi kubwa ya wanaume mkoani Mbeya, wanapenda kulelewa hawapendi kujishughulisha, wanawategemea wanawake kulisha familia na kufanya kila kitu, mbaya zaidi huwashinikiza wake zao kuomba mkopo kwa kutumia account zao ili wadhulumu hizo hela, nawaambia wanawake msikubali kutumika kama ndoa yako ina shida  ondoka kaanzishe maisha mengine”, amesema RC Chalamila.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Ruto Watched Uhuru on TV During BBI Event – Spokesperson

Deputy President William Ruto's team has responded to his conspicuous absence at the BBI event at the Kenyatta International...

Baada ya kifo cha Maradona, Rais atangaza siku tatu za maombolezo

Rais wa Argentina Alberto Fernandez ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha gwiji wa nchi hiyo...

US looting oil, wealth of Syrian people: Iran UN envoy

Addressing a meeting of the UN Security Council on Syria, Majid Takht-Ravanchi said, " After almost 10 years of conflict, the...

UAE suspends issuing visas to citizens of 13 Muslim majority countries

The United Arab Emirates (UAE) has suspended issuing travel and work visas for citizens of 13 mostly Muslim-majority countries,...

Kituo kipya Cha Mabasi kipo katika hali ya kuweza kutumika- RC Kunenge

 Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio leo ambapo Mkuu...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you