News Watano wateketea kwa moto baada ya malori kugongana

Watano wateketea kwa moto baada ya malori kugongana

-

Watu watano wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 21, 2020, mara baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Kitumbi mkoani Tanga, huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Blasius Chatanda, amesema kuwa malori hayo moja lilikuwa likitokea jijini Dar es Salaam likiwa na vifaa vya dukani likielekea mkoani Tanga, na lingine lilikuwa limebeba saruji kuelekea mkoani Dodoma.

“Gari mbili zimewaka moto ni wazi kwamba magari yote haya mawili yalikuwa kwenye mwendokasi, kwa mujibu wa mashuhuda gari moja ilihama kutoka upande wake na ku-overtake gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kugongana, hiyo miili ilivyo ni ngumu hata kufanya utambuzi kwa sababu wameungua vibaya na miili yote imehifadhiwa kwenye kituo cha afya Mkata”, amesema ACP Chatanda.

Aidha ACP Chatanda, akatoa rai kwa madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwa sababu huo ni mwarobaini wa ajali zote za barabarani 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Moscow rolls out Sputnik V Covid-19 vaccine to most exposed groups

Moscow began distributing the Sputnik V Covid-19 shot via 70 clinics on Saturday to the most exposed groups, marking...

Caspian containerized line kicks off between Iran, Russia

TEHRAN, Dec. 05 (MNA) – The activity of Caspian containerized line between Islamic Republic of Iran and Russia’s port...

BDS slams Bahrain’s recognition of Israel settlement goods

The Boycott, Divest and Sanctions (BDS) movement on Friday slammed Bahrain's recognition of settlement goods as "war crimes", Quds...

Abshineh Dam Lake of Hamadan Province

HAMADAN, Dec. 05 (MNA) – Located 15 kilometers away from Hamedan Province in Hamedan-Malayer Highway, west-central Iran, Abshineh pond...

2020 GITEX to host 20 Iranian Knowledge-based firms tomorrow

TEHRAN, Dec. 05 (MNA) – 20 Iranian knowledge-based firms and startups will participate at the 40th international exhibition of...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you