Afrika yaagiza dozi milioni 300 za chanjo ya COVID-19

-

Umoja wa Afrika unatarajia kupata dozi milioni 300 za chanjo ya COVID-19 , ikiwa ni makubaliano makubwa kuwahi kufanyika Afrika. 

Hayo yamesemwa na Nicaise Ndembi, mshauri mkuu wa masuala ya kisayansi katika taasisi ya Afrika yakudhibiti na kuzuia maradhi. 

- Advertisement -

Kwenye mahojiano na shirika la habari la Associated Press, Ndembi amesema rais wa sasa wa umoja huo Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutangaza hatua hiyo leo. 

Ameongeza kuwa dozi hizo milioni 300 ni kutokana na juhudi binafsi za kampuni ya COVAX, kwa lengo la kupelekwa kwa nchi zenye mapato ya chini. 

Hayo yanajiri mnamo wakati maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika yamepindukia watu milioni tatu. 

Afrika Kusinindiyo imeathiriwa zaidi barani Afrika ikiwa imerekodi zaidi ya maambukizi milioni 1.2. Taasisi ya Afrika ya kudhibiti maaradhi ya kuambukiza imesema jumla ya dozi bilioni 1.5 za chanjo ya COVID-19 zinahitajika Afrika na inakadiria kuwa zitagharimu dola bilioni 10.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you