Bunge la Misri laidhinisha uamuzi wa kuongeza muda wa ilani ya hali ya dharura kwa miezi 3 zaidi

-

Bunge la Misri limeidhinisha uamuzi wa kuongeza ilani ya hali ya dharura kwa miezi 3 zaidi kote nchini.

Spika wa Bunge la Misri Hanefi Jibali alitoa hotuba yake katika kikao cha jumuiya na kusema,

- Advertisement -

“Uamuzi wa Rais Abdulfettah al-Sisi wa kuongeza muda wa ilani ya hali ya dharura kwa miezi 3 zaidi kote nchini umekubaliwa na theluthi mbili ya wawakilishi katika Bunge.”

Ilitangazwa kuwa hali ya dharura ambayo iliongezwa kwa mara ya 15 nchini humo, itaanza kutekelezwa kuanzia Januari 24, 2021.

Watu 45 walipoteza maisha na watu 125 walijeruhiwa katika mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa na shirika la kigaidi la DAESH mnamo Aprili 2017 katika miji ya Alexandria na Tanta nchini Misri.

Kufuatia mashambulizi hayo, Rais Sisi alitangaza ilani ya hali ya dharura kwa kipindi cha miezi 3.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you