Goli la dakika ya 82 la mshambuliaji wa Burnley, Ashley Barnes ndiye liliandika historia hiyo baada ya kufunga kwa penalty kufuatia muamuzi wa kati Mike Dean na jopo la waamuzi wa VAR wa mchezo huo kukubaliana mlinda wa Liverpool Alisson Becker alimchezea rafu Barnes.
Mara ya mwisho Liverpool kufungwa kwenye dimba lake la nyumbani la Anfield kwenye EPL, ilikuwa ni tarehe 23 Aprili 2017 walipofungwa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace na bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na mchezaji wao wazamani Christian Benteke.
Baada ya rekodi hiyo kuvunjwa, Kocha wa sasa wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Jose Mourinho atakuwa mwenye furaha kwasababu Liverpool ilikuwa inasaka rekodi ya Chelsea kutofungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani ‘Stamford bridge’ kwa kucheza michezo 86.
Rekodi hiyo ya Chelsea iliwekwa kuanzia mwaka 2004 Aprili hadi Oktoba 2008 na kocha Jose Mourinho, na ndiyo rekodi inayoshikilia namba moja kwa timu kucheza michezo mingi zaidi kwenye uwanja wake wa nyumbani bila kufungwa kwenye EPL.
Kuondoa rekodi ya Liverpool kufungwa Anfield, lakini imeweka rekodi ya kucheza michezo mitano bila kupata ushindi kwa mara ya pili, mara ya kwanza ilikuwa mwezi Januari hadi Februari mwaka 2017 chini ya kochwa Jurgen Klopp.
Baada ya kupoteza mchezo wa jana usiku rasmi sasa Liverpool wanashikilia nafasi ya 4 kwa kuwa na alama 34, alama 6 nyuma ya vinara Manchester United ingawa siku ya Jumapili Manchester United wanaikaribisha Liverpool kwenye mchezo wa FA ambao hautakuwa na madhara kwa United kwenye ligi pia hata kama Liverpool watashinda hautawasaidia kwenye msiamo wa ligi.