Connect with us

Hi, what are you looking for?

Muhabarishaji News

News

DC Jokate akuta madudu TANESCO

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za TANESCO wilayani humo na kukutana na malalamiko lukuki toka kwa wananchi waliofika katika ofisi hizo wakidai kucheleweshewa kuwekewa umeme majumbani mwao ikiwemo kero ya kukatika katika kwa umeme.

Majira ya saa tatu asubuhi DC Jokate, alifika katika ofisi za TANESCO wilaya na kukutana na wananchi waliofika mahala hapo wakisubiri huduma na kupata fursa ya kusikiliza kero ya wananchi hao, huku wengi wao wakilalamikia hasara wanayoipata pindi umeme unapokatika.

Mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi hao na kujiridhisha, DC Jokate, akaagiza kuswekwa rumande kwa baadhi ya watendaji wa idara hiyo huku akiutaka uongozi kuhakikisha inatatua kero inayowakabili wananchi haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wa viongozi wa TANESCO licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto hizo lakini wakaahidi kuanza kuyafanyia kazi mapungufu hayo mara moja.

Click to comment

Leave a Reply

You May Also Like

Health

Life is full of struggles—some easy, some tough. We may struggle to wake up in the morning or study for an upcoming test. We...

Music

DOWNLOAD Listen to Stamina Ft. Atan – ASIWAZE byDJ Mwanga on hearthis.at

News

Jina Lake Kamili Anaitwa Joseph Roy Metheny, Alizaliwa March 2, 1955 Huko Maryland US na Kufariki Akiwa Gerezani Augost 5, 2017 Akiwa na Umri...

Music

It’s a brand new day and we are happy to bring you a brand new hit song titled I like it by Darassa Ft....