Harmonize: Ntamsaidia Anjella kwa namna yeyote licha ya kuwa na ulemavu, alikuwa anatengwa

-

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amepost picha ya Anjella na kuandika maneno haya:
“Niliumbia Moyo Wangu Kwamba Siwezi Ona Kipaji Cha Huyu Dada Kinateketea Eti Kwasababu Tuu Anaulemavu Ambao Amebarikiwa Na Mungu Ambae Kazi Yake Haina Makosa …!!! Na Hajawahi Kukosea..!! Na Hakuna Mwenye Haki Ya Kuikosoa Iwe kwenye Jua Mvua Nitahakikisha Kipaji Chake Kinawafikia ..!!! Mtaamua Nyinyi Kumuunga Mkono Au Laaa …!!!! Nimemshirikisha Kwenye Wimbo Wangu Wakwanza Kabisa…!!! Mwaka 2021 it’s Worldwide 🌐 Sound Ninaimani itamfungulia Milango Mingi Na Kuifikia Ndoto Yake Alioikimbilia Kiujasiri ..!! Na Kujiamini Bila Kujali Mapungufu Ama Ulemavu Aliotunukiwa Na Mungu Wenda Ingekuwa Sababu Ya Kukata Tamaa na Ukizingatia Ni Mtoto wa Kike …!!! TAFADHALI SEMA NENO LOLOTE LA KUMTAKIA SAFARI NJEMA katika Kuikimbilia Ndoto Yake Iliyo Moyoni …!!!! 🙏 “

Baada ya post hiyo Anjella aliandika ujumbe huu.
“Eeeh mwenyezi mungu nakushukuru kwa kunikutanisha na huyu kaka @harmonize_tz kupitia yeye umeniheshimisha kwakwel nina furaha ambayo sikuwahi kuipata mwanzo maisha yangu yalikua yakutengwa kutokana na ulemavu niliokua nao amani na furaha niliyokua nayo sasa siwezi elezea nakushukuru MUNGU nakushukuru @harmonize_tz 🙏🙏🙏”

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you