Huyu hapa atajwa kuwa mrithi wa David Kissu

-

 

NASRI Talib kipa namba moja wa Klabu ya Jamhuri ya Zanzibar anatajwa kuingiza kwenye rada za Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina raia Zambia.

Talib alikuwa kizuizi kwa Yanga kupata ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan baada ya kuwa imara ndani ya dakika 90 kwa kuzuia michomo ya washambuliaji wa Yanga na kufanya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

- Advertisement -

Azam FC iliishia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuondolewa na Yanga kwa kufungwa penalti 5-4.

Dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo kipa namba tatu Wilbol Maseke alitunguliwa na Tuisila Kisinda huku Farouk Shikalo yeye akitunguliwa na Obrey Chirwa.

Kipa namba mbili Benedict Haule aliishia kuokoa penalti moja pekee iliyopigwa na Michael Sarpong huku tano zote zikizama ndani ya nyavu.

Kipa namba moja David Kissu amekuwa akifanya pia makosa ya mara kwa mara jambo ambalo limewafanya mabosi hao kufikiria kumuongeza nyota huyo ndani ya kikosi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ikiwa kutakuwa na pendekezo la kumsajili mchezaji watampata kwa kuwa bado dirisha dogo halijafungwa na usajili upo kwa ajili ya timu kubwa.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you