Kigonya amesaini dili la miaka miwili Azam FC

-

 

MATHIAS Kigonya raia wa Uganda kwa sasa ni mali ya Azam FC akiwa amesaini dili la miaka miwili yeye ni kipa alikuwa anakipiga ndani ya Forest Rangers ya Zambia.

Sasa ndani ya Azam FC orodha ya makipa inakuwa ni watatu ndani ya kikosi cha kwanza ambao ni David Kissu, Benedict Haule pamoja Kigonya.

- Advertisement -

Wote wakiwa chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina raia wa Zambia wana kazi ya kuonyesha ubora wao ili kujihakikishia namba kikosi cha kwanza.

Habari zinaeleza kuwa huenda mmoja kati ya makipa hao akatolewa kwa mkopo ndani ya timu hiyo ama kuvunjiwa mkataba ambapo kwa makipa jina anatajwa kuwa ni David Kissu.

Pia kuna mpango wa nyota wa kikosi hicho Richard Djod naye kutolewa ndani ya kikosi hicho kumpisha mshambuliaji Mpiana Monzinzi ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mpango mkubwa wa kikosi hicho ni kuwa bora muda wote na kuleta ushindani.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you