Kisanduku cha pili cha ndege iliyoanguka Indonesia chapatikana

-

Shughuli ya utafutaji bado inaendelea katika eneo la ajali ya ndege ya abiria iliyoanguka baharini muda mfupi baada ya kuruka siku ya Jumamosi nchini Indonesia.

Baada ya kisanduku cheusi (kisanduku cha mawasiliano ya ndege) kupatikana katika utaftaji uliofanyika hapo jana, taarifa muhimu zinatarajiwa kupatikana kutoka kwenye vifaa hiyvo viwili na kusaidia kugundua chanzo cha kuanguka kwa ndege.

- Advertisement -

Kwa upande mwingine, maafisa wa hospitali walisema kwamba idadi ya mifuko iliyo na sehemu za mwili zilizopatikana ilifikia 137, na mali za kibinafsi zilikusanywa katika mifuko 35.

Katika vipimo vya DNA vilivyofanywa, ilitangazwa kuwa jumla ya watu 4, ikiwa ni pamoja na rubani msaidizi, mhudumu 1 na abiria 2 waliweza kutambuliwa hadi kufikia sasa.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hapo jana, Waziri wa Uchukuzi Budi Karya Sumadi alitangaza kuwa mawasiliano yalikatishwa takriban dakika 5 baada ya kuruka kwa ndege ya abiria ‘SJ182’ iliyokuwa na wafanyikazi 12 na abiria 50, na kuangukia katikati ya Kisiwa cha Laki na Lancang, upande wa kaskazini mwa mji mkuu Jakarta.

Jeshi la Wanamaji la Indonesia limesema mabaki ya ndege ya abiria yalitawanyika katika sehemu 4 tofauti kutoka Visiwa vya Thousand Islands, kaskazini mwa pwani ya mji mkuu wa Jakarta.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii ya Flightradar24 ambayo inafuatilia ndege za ulimwengu, ilisema kwamba ndege hiyo ilifikia takriban futi 11,000 (mita 3,352) dakika 4 baada ya kuruka, kisha ikaanguka futi 250 chini ya dakika 1 na kupoteza mawasiliano na kituo cha kudhibiti trafiki angani.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you