Kiwanda cha dangote kuanza uzalishaji Jauari 11

-

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

- Advertisement -

Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dongote kilichopo kata ya mayanga Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara kitanza rasmi uzalishaji wake kuanzia siku ya juma tatu tarehe 11 Januri 2021.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alipotembelea kiwandani hapo na kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa kiwanda hiko Ndg Abullahi baba aliyotoa mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa sababu iliyopelekea kiwanda hiko kusitisha uzalishaji wake kwa wiki kadhaa ni pamoja nyufa iliyotekea katika mtambo mmojawapo ndani kiwanda hiko ambapo kifaa kilichotakiwa kufungwa hakikopatikana nchini bali kiliagizwa kutoka nchini India hali iliyopelekea kusitisha uzalishaji wa saruji kwa wiki kadhaa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai kwa wafanyabishara wa uuzaji wa saruji kuacha kupandisha bei ya saruji kwa kipindi hiki kwa kisingizio cha kutopatikana kwa bidhaa hiyo kwani kufanya hivyo kuwakosea watanzania .

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hiko Ndg Abullahi Baba ametoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano alionao haswa katika kipindi ambacho kiwanda hiko kinapokuwa na changamoto katika uendashaji wake.

Lakini Ndg Baba ameendelea kutoa wito kwa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei kwani kuanzia juma tatu kiwanda hiko kinaanza rasmi kuzalisha zaruji na kusamba hapa nchini.

Baba ameendelea kusema kuwa mara bada kiwanda hiko kuanza uzalishaji wake bado watendelea kuuza kwa bei rafiki ili watanzania waweze kupa fursa ya kujenga nyumba zao.  

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you