Mnisamehe, sitorudia – Mkude awaangukia mabosi zake (+Video)

-

Baada ya Klabu ya Simba kumsimamisha kiungo mkabaji, Jonas Mkude kwa muda usiojulikana na sababu kubwa ikielezwa ni masuala ya kinidhamu.

Kuangalia Video bofya HAPA

- Advertisement -

Hatimaye mchezaji huyo ameliomba radhi benchi la ufundi, wachezaji, wanachama na mashabiki bila kusahau Uongozi wa klabu hiyo.

”Tumeumbwa kukosea lakini haimaanishi nitakosea tena,, Mm ni Mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu!!”

”Naamini Wachezaji wenzangu,Benchi la ufundi,Viongozi,Wanachama na Washabiki mtanielewa na mtanisamehe,,”

Disemba 28, 2020 Klabu ya Simba kupitia mitandao ya kijamii ilitoa taarifa ya kumsimamisha kiungo huyo kutokana na utovu wa nidhamu.

Kupitia mitandao ya kijamii ya Simba wametoa taarifa inayoeleza;  “Tunasikitika kuwaarifu wanachama, mashabiki wa klabu ya Simba na wapenzi wote wanaitakia kheri klabu ya Simba kuwa mchezaji Mkude amesimamishwa.”

“Mchezaji Mkude amesimamishwa kutokana na pamoja na mambo mengine tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili,” imeeleza taarifa hiyo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you