Papa Francis afanyiwa chanjo ya Covid-19

-

 

Kiongozi wa kiroho wa Wakatoliki na Rais wa Vatican, Papa Francis, amefanyiwa chanjo iliyoboreshwa dhidi ya virusi vya corona (Covid-19).

- Advertisement -

Msemaji wa Vatican Press Matteo Bruni alisema,

“Ninaweza kuthibitisha kwamba Baba Mtakatifu Papa Francis amepewa dozi ya kwanza ya chanjo kama sehemu ya mpango wa chanjo ulioanzishwa na Jimbo la Utawala la Vatican.”

Bruni aliongezea kusema kuwa mtangulizi wa Papa Francis ambaye ni Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 93, pia alifanyiwa chanjo ya Covid-19.

Kampeni ya chanjo ya Covid-19 ilizinduliwa jana huko Vatican.

Papa Franciscus, alisema kwenye mahojiano yaliyochapishwa mnamo Januari 9,

“Ninaamini kimaadili kwamba kila mtu anapaswa kupewa chanjo. Hili ni chaguo la kimaadili kwa sababu sio sahihi kucheza na afya yako na kuweka maisha yako na ya wengine hatarini.”

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you