Alexei Navalny apigwa faini kwa “kumkashifu” mkongwe wa vita vya pili vya dunia nchini Urusi

-

 

Mahakma nchini Urusi imetoa uamuzi wa kesi ya pili iliyokuwa ikimkabili kiongozi wa upinzani Alexei Navalny. 

- Advertisement -

Navalny, alipatikana na hatia ya kumkashifu mkongwe mmoja aliyeshiriki kwenye wa vita vya pili vya dunia na hivyo ametakiwa kulipa faini ya karibu Euro 9,500. 

Kabla ya hapo, mahakama ilitupilia mbali rufaa ya kesi yake nyingine aliyowasilisha kupinga umauzi wa kumfunga jela miaka mitatu kwa kosa la kukiuka dhamana. 

Wafuasi wake wanadai kuwa mashtaka yote mawili ni njama ya kisiasa ambapo serikali inataka kuunyamazisha upinzani dhidi ya rais wa Urusi Vladimir Putin.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you