Biteko: Uwazi Uwepo Ili Wawekezaji Wapate Faida Kwenye Madini

-

 

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amesema kuwa Serikali inatamani sekta ya madini iwe rafiki kwa wachimbaji wote kwa kufanya kazi kwa uwazi ili kila aliyewekeza fedha yake imrudishie faida.

- Advertisement -

Biteko amebainisha hayo leo Jumatatu kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini Tanzania wakati akimkaribisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu kutoa neno la ufunguzi.

Biteko amesema kuwa wao kama viongozi watahakikisha wanawaelekeza na kuwalea ili malengo hayo iliyojiwekea Serikali yapate kufikiwa.

“Sekta hii asilimia 90 inaendeshwa na sekta binafsi waliamua  kuwekeza fedha zao  kwa ku ‘risk’ ili Serikali ipate kodi ni lazima tuwalee kwa kuhakikisha mahusiano yetu yanakuwa mazuri” amesema Biteko.

Aidha, Biteko ametoa ahadi ya kuwashughulika na wale wote wanaorudisha sekta hiyo nyuma mmoja mmoja ili kufuta mtazamo hasi uliojengeka katika jamii kuwa watu wote wanaojishughulisha na sekta hiyo ni wahalifu.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you