DC Msafiri ashtukia hujuma za wafanyabiashara kwa wakulima wa Parachichi

-

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kufuatia ununuaji holela  wa tunda la parachichi unaoendelea mkoani Njombe ,mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amehitaji kupangwa bei elekezi ya zao hilo ili kuwaepusha na unyonyaji unaoweza kufanywa na wanunuzi kwa wakulima .

- Advertisement -

Msafiri amesema kumekuwa na wanunuzi wanaonunua shilingi 1,200 ,1,500 na wengine 1800 kwa kilo jambo ambalo linaweza kuwafanya wakulima kukosa tija na maendeleo kwa uwekezaji wanaofanya katika kilimo hicho chenye soko la uhakika ulimwenguni.

Akizungumza wakati wa hafra ya wadau wa parachichi waliokutanishwa na asasi ya TAHA kwa kushirikiana na MAKEUP kwa ajili ya kujadili kuhusu upataji wa cheti cha ithibati ya viwango vya kimataifa GROBAL GAP na ushuhuda wa baadhi ya wakulima waliopata ithibati. Mkuu huyo wa wilaya amesema ni vema wafanyabiashara kuwekewa bei elekezi pamoja kuundwa kwa ushirika ili kudhibiti  unyonyaji.

“Kuna changamoto kubwa ambayo mimi naiona inaenda kuua parachichi badala ya kuiendeleza,wanunuzi kwenda mpaka shabani kwa wakulima naona ni changamoto kubwa,niwaombe TAHA mtuanzishie masoko ili mkulima akivuna aende soko lilipo na wanunuzi waje kununulia hapo,hao wanunuzi wanaofuata mkulima mmoja mmoja hawatendi haki”alisema Ruth Msafiri

“Lakini tukiwa na soko wakulima walete mazao yao wenyewe ndani ya kontena ambazo zimeandaliwa na anapoleta hapo tunakuwa na soko la kuzindua msimu ili wanunuzi washindane na wanunue kwa bei nzuri.nashangaa wakulima wamerizika sijapata mkulima hata mmoja ila mimi moyoni naliona haliko sawa”aliongeza Msafiri

Akifafanua manufaa ya kuwa na vyeti vya ithibati, kimataifa afisa kilimo,afya ya mimea wizara ya kilimo Musa Chidinda anasema  hatua hiyo itasaidia wakulima wanaoyofanya kilimo biashara kuyafikia masoko huku Safari Fungo mratibu wa mradi wa MAKEUP akieleza pia faida ya kuwa na umoja wenye nguvu.

“Zipo faida za kuwa ndani ya Chama cha watu wa parachichi,na ndio tutaona namna mbinu za kibiashara zitawekwa lakini pia wasafirishaji wanayo nafasi kubwa ya ushiriki kwenye hili”alisema Safari Fungo

“Pamoja na hilo tunawasaidi wakulima kupeleka tunda sokoni,mwaka 2020 kwa kushirikiana na TAHA tuliwapeleka wasafirishaji wa parachichi kwenye maonesho nchini Ujerumani.sasa hivi tumewasaidi na wakulima wanauza kilo moja kwa dola 10 kutoka dola 2.kwa hiyo sisi kazi yetu ni kuwasaidia wakulima wapate zaidi matunda kupitia mbinu za kutafuta ubora lakini pia kuongeza thamani kwenye mazao yao”aliongeza Safari Fungo

Steven Mlimbila maarufu kwa kilimo cha parachichi kwa jina la Nemes na Zakia Luwanja ambao ni wakulima wa parachichi wanasema bei elekezi itasaidia kudhibiti unyonyaji kwa wakulima huku wakibainisha changamoto ya miundombinu ya barabara na maji kukwamisha uwekezaji wao.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you