Diana Madukwa: Tuna Rais mwenye hofu ya Mungu

-

KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa ameunga mkono kauli ya Rais Dk John Magufuli ya kuwahimiza watanzania kufanya maombi akisema kuwa huo ni uthibitishonwa jinsi gani Tanzania ina kiongozi mwenye maono na mwenye hofu na Mungu.

Madukwa amesema katika kipindi hiki ambacho watanzania wengi wamekua na hofu inayosababishwa na kutishwa na watu wasio na mapenzi mema juu ya ugonjwa wa kushindwa kupumua, Rais Dk Magufuli ametoa kauli iliyozalisha tumaini jipya kwa watanzania walio wengi.

- Advertisement -

Amesema hata mwaka jana wakati ugonjwa huo ukishika kasi sehemu mbalimbali duniani, Dk Magufuli alisimama na kuwataka watanzania kila mmoja kwa imani yake kumuomba Mungu jambo ambalo lilisaidia kuondoa ugonjwa huo na kusaidia Tanzania kuendelea na shughuli zake za kiuchumi bila Rais kufungia watu ndani kama Nchi zingine zilivyokua zikifanya.

” Ni haya haya maombi ambayo Rais Dk Magufuli amesema tuyafanye ndio alituhimiza mwaka jana tuyafanye na tukaushinda ugonjwa huu kiasi kwamba tukawa tunaendelea na shughuli zetu bila kufungiwa na uchumi wetu ukapaa hadi kufikia uchumi wa kati, hivyo naungana na Rais wetu mpendwa ya kwamba maombi ndio njia pekee ya kuishinda hofu tuliyonayo.

Maombi yanaondoa hofu, kwa sababu hofu ndio husababisha hata magonjwa mengine kuibuka hata presha, kwa sababu hofu inamletea mtu msongo wa mawazo lakini ile kuondoa hofu inamsaidia mtu kuondokana na presha, lakini kupitia kauli ya Rais kuwa hatofungia watu ‘lockdown’ inachangia watu kuendelea kufanya kazi na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na uchumi wa Nchi kama tulivyofanikiwa mwaka jana kiasi cha kufikia uchumi wa kati,” Amesema Madukwa.

Ametoa wito kwa watanzania kwa umoja wao kuungana na Rais Dk Magufuli kufanya maombi kama ambavyo amesisitiza kwani itasaidia kuondoa hofu inayoletwa na watu kwani kupitia Maombi Mwenyezi Mungu atalivusha Taifa letu kama ambavyo alituvusha mwaka jana.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you