DR Congo yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola Butembo

-

DR Congo ilikuwa imehifadhi chanjo kwa ajali ya matumizi ya dharura, maafisa wamesema

Kampeni ya chanjo ya Ebola imeanzishwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi huu, Shirika la Afya Duniani – WHO limesema.

- Advertisement -

DR Congo imethibitisha visa vinne vya ugonjwa wa Ebola tangu kutangazwa kwa mlipuko mwingine wa virusi hivyo Februari 7 huko Butembo.

Wafanyakazi wa afya katika vituo vya afya ambako mgonjwa wa kwanza wa Ebola alitibiwa walikuwa wa kwanza kupata chanjo, WHO imesema.

Taarifa hizo zinawadia baada ya Guinea iliyopo Afrika Magharibi kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you