Familia ya mchungaji mtoro wa Malawi ‘yazuiliwa uwanja wa ndege’

-

Familia mchungaji milionea wa Malawi mwenye utata, Shepherd Bushiri, imezuiliwa katika uwanja wa ndege nchini humo ilipokuwa ikijaribu kusafiri kwenda Kenya, kituo cha habari cha eNCA Afrika Kusini,kimemnukuu wakili wa familia.

Bw. Bushiri na mke wake Mary,wanakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha na udanganyifu nchini Afrika Kusini.

- Advertisement -

Walikiuka masharti ya dhamana waliyopewa Novemba mwaka jana na kukimbia nyumbani kwao Malawi.

Wakili wa familia aliyenukuliwa na kituo cha eNCA amesema mabinti wa Bw. Bushiri na mama mkwe wake walizuiliwa kuondoka Malawi kwenda Kenya.

Mabinti zake walikuwa wanaenda kutafuta huduma za matibabu.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you