Keboye Tumuenzi Mwalimu Nyerere Kwa Vitendo Na Kutembelea Makumbusho Ya Nyumbani Kwake Ili Kujifunza

-

 

Na Timothy Itembe Mara.

BAADHI ya wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) wilayani Tarime wamemwagia sifa  uongozi wa mkoani Mara kwa kutekeleza ahadi kwa wananchi wake.

- Advertisement -

Moja ya changamoto iliyokuwa ikiwangisha vichwa Chama hicho ni pamoja na namna gani wataende kushinda uchaguzi wa mwaka 2020 na majimbo ya halmashauri za mkoani hapa kuongozwa na CCM.

Akiongea kwa niaba ya wenzake katibu itikadi na uwenezi kata ya Turwa,Kichichi Marwa Kesanta alisema kuwa wamepata tabu sana pindi majimbo ya halmashauri ya Tarime mjini pamoja na Tarime vijijini yakiongozwa na wapinzani kwa maana ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Kichichi alisema kuwa wanachama wa Chama cha mapinduzi kwa ujumla wanampongeza Rasis wa Jasmhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kukirudishia chama hicho heshima na wananchi kukiamini na kuwapatia kura ya kuongoza.

“Moja ya sifa tuliyojikusanyia kutoka kwa viongozi wetu ni pamoja na utekelezaji wa miradi kwa wananchi ambayo inatekelezwa kupitia awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli jambo ambalo wanachama wa Chama cha mapinduzi tunatembe kifua mbele”alisema Kichichi.

Pia Mwenezi huyo alisema baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wanatumia rfusa hiyo kumpongeza mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoani hapa,Samweli Keboye kutekeleza ahadi aliyoitoa mbele ya viongozi wa ngazi ya juu wa Chama chake kuwa atahakikisha anakomboa majimbo ya mkoa Mara na kurudi CCM ambapo imetekelezwa na sasa halmashauri zote zinaongozwa na Chama cha mapindizu.

Sifa nyingine ya Keboye na ambayo ni ahadi ndani ya chama chake ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi hayapo na anashugulikia hatua ya kuwaunganisha wanachama wote ili kuwa kitu kimoja katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 20/25 ya Chama cha mapindizu ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Naye mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoani hapa,Samweli Keboye maarufu namba tatu amekuwa na ari ya kuona Chama chake kupitia viongozi wake wanakemea Rushwa ambayo niadui wa haki ambapo rushwa inarudisha nyuma usitawi wa jamii kwa ujumla.

Namba Tatu amekuwa mstari wa mbele kuona haki kwa jamii inatendeka na chama chake hakichafuliwi kwa namna yeyote ile na kuwa  viongozi wake wanatembe kifua mbele wakinufaika na matunda ya Tanzania pamoja na  uhuru wake u;liotokana na  juhudi za mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa hatua nyingine namba Tatu alisema jamii iendelee kumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo na isiwe kwa maneno huku wakitembelea familia yake kuwatia nguvu ikiwemo kutembelea makumnbusho yake kwa lengo la kujifunza 

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you