Kisa mtoto wa Kajala, Harmonize amvaa Rayvany “Ulipata wapi ujasiri huu wa kutembea na mwanafunzi”

-

Ni ‘headlines’ za sakata la video ambazo zimeonesha msanii wa kiume na mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja na P-Funk Majani aitwaye ‘Paulah Kajala’ wakiwa wana-kiss kwenye gari ambapo Harmonize amevunja ukimya na kuhoji kwa alichokifanya msanii huyo.

Kupitia ‘Insta Post’ yake msanii Harmonize ameandika ujumbe mzito unaohusu sakata hilo juu ya msanii huyo kumrekodi video Paulah Kajala ambaye bado ni mwanafunzi.

- Advertisement -

“Ulipata wapi ujasiri huu wa kutembea na mwanafunzi wa kidato cha (5) wakati ni wazi kwamba ni kosa la jinai na hukumu yake sio chini ya miaka 30, lakini pia isitoshe una-record video ukiwa una-kiss unaonesha kwamba Serikali haiwezi kukufanya kitu, nawaza lengo lilikuwa ni kuonesha upo juu ya sheria ama” 

“Hebu angalia ‘future’ ya mtoto wa watu umeiweka wapi kwa tamaa za siku 1, kama kweli mlikuwa mnapendana mpo ‘in love’ video ilikuwa na haja gani na lengo la kuvujisha ni nini, lakini pia Serikali  itajiuliza una videos ngapi za watoto wa shule kama umeweza kuwa na hii ukaivujisha” ameandika Harmonize 

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you