KMC FC yaanza kujifua dhidi ya michuano ya kombe la shirikisho

-

Mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Kagera Sugar, Timu ya KMC FC leo imeendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa michuano ya kombe la Shirikisho ASFC sambamba na michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara ambapo itakuwa ugenini dhidi ya Polisi Tanzania pamoja na Coast Union ya Tanga.

KMC itacheza mechi ya kombe la Shirikisho ASFC  Ijumaa ya Februali 26 dhidi ya Timu ya Kurugenzi ya Mkoani Simiyu utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine vijana wa Kino Boys wamejipanga kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri na hivyo kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

- Advertisement -

Aidha KMC itakuwa ugenini katika michezo yake miwili ambapo itakutana na Polis Tanzania Marchi nne katika uwanja wa Sheim Amri  Beid Mkoani Arusha ,huku mechi dhidi ya Coast Union ikipigwa Machi saba katika uwanja wa Mkwawani mkoani Tanga.

 “Tumemaliza mechi yetu ya Ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, na sasa tunajipanga katika mchezo wa kombe la ASFC, tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na kwamba wapinzani wetu ndio tunakutana nao kwa mara ya kwanza, hivyo tunajipanga ilituweze kupata matokeo katika mchezo huo.

 “ Tulifaya vizuri katika michezo yetu mwili ambayo tulikuwa nyumbani, sasa tunakwenda kucheza michezo yetu mwili tukiwa ugenini, ligi ni ngumu na tunafahamu kuwa kila Timu inahitaji matokeo, lakini kama KMC FC tunapambana kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri katika michezo yetu hiyo miwili.

Hadi KMC FC po katika nafasi ya tano ikiwa imecheza michezo 21 na kufikia alama 31 , hivyo mkakati ni kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo inayofuata na hivyo kuendelea kupanda katika nafasi za juu.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you