Maambukizi mengine ya mafua ya ndege yaibuka

-

 Wakati dunia ikihaha kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, Urusi imeripoti aina ya virusi vinavyosababisha mafua ya ndege kwenda kwa binadamu, kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), Reuters imeripoti.

Mataifa mbalimbali duniani kwa sasa yameanza kuwapa wananchi wake chanjo ya Covid-19 baada ya ugonjwa huo wa homa ya mapafu kuua zaidi ya watu milioni moja kote duniani na kusababisha WHO itangaze janga hilo kuwa dharura ya dunia.

Anna Popova, mkuu wa afya ya wateja wa taasisi ya Rospotrebnadzor, alisema Jumamosi kuwa Urusi imeripoti virusi hivyo vinavyoitwa A(H5N8) kuwa vinaambukizwa kwa binadamu.

- Advertisement -

Mlipuko wa jamii hiyo ya virusi ya H5N8 umeripotiwa nchini Urusi, barani Ulaya, China, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika miezi ya karibuni, lakini hadi sasa ni kwa kuku tu, imeripoti Reuters.

Aina nyingine za virusi vya H5N1, H7N9 na H9N2 zinajulikana kuwa zinasambaa kwa binadamu.

Kwa mujibu wa Reuters, Urusi iliripoti maambukizi kwa binadamu siku kadhaa zilizopita, “mara tu baada ya kuwa na uhakika wa matokeo,” Reuters imemkariri Popova akiongea na kituo cha televisheni cha Rossiya 24 kinachomilikiwa na serikali.

Hata hivyo, bado hakuna dalili za binadamu kwa binadamu kuambukizana virusi hivyo, alisema.

Wafanyakazi saba katika shamba la kuku kusini mwa Urusi waliambukizwa virusi vya H5N8 katika mlipuko eneo hilo mwezi Desemba, alisema Popova.

Hata hivyo walioambukizwa wanaendelea vizuri, “Hali hii haikukua zaidi,” alisema.

Katika barua pepe, WHO ilisema imetaarifiwa na Urusi kuhusu maambukizi hayo kwa binadamu na kuthibitisha kwamba jambo hilo litakuwa la kwa aina hiyo ya virusi kumuingia binadamu.

“Taarifa za awali zinasema kuwa walioambukizwa walikuwa wafanyakazi katika eneo la ndege,” imesema barua pepe hiyo.

“Tuko katika mazungumzo na mamlaka za taifa kwa ajili ya kukusanya taarifa na kutathmini afya ya umma katika tukio hili.”

Maambukizi ya mafua ya ndege yamekuwa yakihusishwa na watu wanaofanya kazi moja kwa moja na viumbe hao wakiwa hai au waliokufa, lakini chakula kilichopikwa vizuri kimekuwa kikichukuliwa kuwa salama.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you