Meli mbili za walinzi wa pwani ya Wachina ziliingia kwenye maji ya eneo la Japan kuzunguka Visiwa vya Senkaku vinavyozozaniwa katika Bahari ya Mashariki ya China.
Kulingana na Makao Makuu ya Walinzi wa Pwani wa eneo la 11 wilayani Naha mkoani Okinawa, upande wa kusini magharibi mwa Japan, meli za China zilikiuka mipaka ya bahari ya kitaifa.
Karibia saa 4:50 za asubuhi kwa saa za karibu na visiwa vya Senkaku, meli zilikiuka sheria na kukaribia boti za Uvuvi za Japan zilizokuwa zikivua karibu na kisiwa cha Kuba-jima.
Boti za uvuvi zililindwa na meli za Walinzi wa Pwani wa Japan zilizotumwa katika mkoa huo.
Meli za Wachina zilionywa kuondoka katika eneo hilo.
Kulingana na kanuni za makao makuu, meli za Wachina zimekiuka sheria za mipaka ya bahari na ardhi ya Japani katika maeneo ya karibu na Senkaku mara 9 hadi sasa ndani ya mwaka huu.