Mkutano uwekezaji sekta ya madini kuanza kesho

-

Mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini, wenye lengo la kukuza uwekezaji na kuwakutanisha wadau wa uchimbaji na wafanyabiashara ya madini, unatarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere.

- Advertisement -

Mkutano huo wa tatu kufanyika nchini, wenye kauli mbiu isemayo sekta ya madini kwa uchumi imara na maendeleo endelevu, utawahusisha wazawa na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi ambapo asilimia kubwa ya wageni watahudhuria kwa njia ya video mtandaoni.

Akizungumza wakati wa maandalizi leo Februari 21, 2020, Naibu Waziri wa Madini Profesa Shukrani Manya amesema mwitikio ni mzuri na kwamba mkutano huo unawahusisha watu wa ndani ya nchi na nje ambao wapo waliofika na wengine watashiriki wakiwa katika nchi zao kwa njia ya video conference.

“Mkutano huu una malengo ya kukuza uwekezaji katika sekta ya madini kwa maana tunawahitaji  wawekezaji kutoka nje ili kuleta fedha za kigeni na kuwekeza mitaji yao katika nchi yetu na moja ya salamu tunayowapa, Tanzania ni mahali pazuri kuwekeza mtaji wako ukapata faida na ni mahali sahihi pa kuwekeza,” amesema.

Profesa Manya ametaja lengo jingine kuwa ni kuwakutanisha wadau wa uchimbaji na biashara ya madini waliopo hapa nchini waweze kupata muda wa kujadiliana na Serikali yao, zikiwemo taasisi, wizara na wengineo wanaohusika na madini.

“Mjadala huu ulifanyika mwaka 2019 wakati Rais John Magufuli alipogeuza uliokuwa mkutano kuwa kikao na wachimbaji wadogo na matokeo katika mkutano huo yalisaidia kuondoa kodi ya zuio la asilimia 5 ya madini pamoja na asilimia 18 ya kodi ya ongezeko la thamani ambayo yalipelekea ustawi katika sekta ya uchimbaji mdogo nchini.

“Baada ya matokeo bora tunaona madini yakaanza kuingia kwa wingi katika masoko yetu hivyo uchimbaji mdogo ukaanza kuchangia kwa sehemu kubwa ya mapato yatokanayo na madini,” amesema Profesa Manya.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you