Mwanasisa wa upinzani wa Rwanda auawa Afrika Kusini

-

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Ripoti zinasema Seif Bamporiki aliuawa alipokuwa akiwasilisha samani kwa mteja Jumapili mchana mjini Cape Town. Haijabainika kama kifo chake kilichochewa kisiasa.

- Advertisement -

Waliomvamia walichukua simu zake za rununu na waleti kabla ya kutoroka eneo la tukio.

Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Bw. Bamporiki alikuwa mshirikishi wa chama cha Rwanda National Congress.

Msemaji wa chama hicho, Etienne Mutabazi, ameiambia BBC kwamba mteja alikuwa amewasiliana na Bw. Bamporiki – ambaye anaendesha duka la kuuza vitanda – kuuliza kama ana kitanda cha kuuza.

Mteja kisha aliomba kitanda hicho kupelekwa katika mji wa Nyanga na kuamua kutumia gari na Bwana Bamporiki na mwenzake kwenda eneo ambalo kitanda kilitakiwa kupelekwa.

Maelezo ya kile kilichotokea baada ya hapo bado hayajathibitishwa, lakini Bw. Bamporiki aliuawa kwa risasi moja ambayo ilipigwa kupitia dirisha la gari.

Mji wa Nyanga unafahamika kuwa moja ya miji hatari nchini Afrika Kusini.

Wakati mmoja ulikuwa na idadi ya juu zaidi ya mauji kwa mwaka.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you