Mzozo wa Tigray: Msaada mkubwa wa kibinadamu unahitajika

-

Mahitaji ya watu walioathirika na mapigano ya jimboni Tigray nchini Ethiopia ni ”makubwa mno”, Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limetahadharisha.

”Watu wa Tigray… wamepoteza msimu wa mavuno,” Mkurugenzi wa operesheni wa ICRC, Dominik Stillhart, ameiambia BBC wakati wa ziara yake Ethiopia.

- Advertisement -

Alisema kuwa kulikuwa na ” masuala muhimu yanayohusu huduma za afya” kuwafikia wahitaji.

Serikali ya Ethiopia awali ilisema kuwa watu milioni 1.5 walifikiwa.

Maelfu ya watu wanaripotiwa kuuawa na karibu milioni mbili wameyakimbia makazi yao.

Karibu wakimbizi 100,000 wa Eritrea waliokuwa wakiishi katika makambi ya wakimbizi ya UN katika jimbo Tigray wamenasa katika mzozo huo.

Mzozo uliibuka mwezi Novemba baada ya chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kudhibiti kambi kadhaa za kijeshi Tigray baada ya kuvunjika kwa mahusiano na serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed mjini Addis Ababa.

Serikali kuu- ambayo imejitangazia ushindi- ilizuia kuingia Tigray hasa vyombo vya habari na mashirika ya misaada.

- Advertisement -
Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you